Ali Mango akiwa katika picha ya wimba ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), alisema vazi hili ni maalumu kwa kucheza na Nyoka.
Ali Mango ambaye pia ni mtaalamu wa kucheza na nyoka kama tujuavyo Wanyamwezi na Wasukuma katika ngoma xzao lazima kitu cha Chato lazima kiwakilishe na ngoma inoge lazima kiwepo. Ali Mango ni mmmoja kati ya wasanii waliopata udhamini na Ubalozi wa Marekani ambaye atakuwa miongoni mwa waasisis na wasanii watakaounda beni itakayokuwa na vionjo vya asili ya makabila ya Kanda ya Ziwa yaani Wasukuma na Wanyamwezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions , Amon Mkoga. http://www.chief/ promotions .or.tz 0755638004/0655638004.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakipata ufafanuzi wa jambo fulani kutoka kwa Ali Mango MAELEZO, Dar es Salaam leo asubuhi.
Amon Mkoga akionyesha kijarida kilichokuwa na matukio ya tamasha la Mtemi Milambo lililofanyika Julai mwaka huu mkoani Tabora.
WASANII wa Muziki wa saili walioshiriki katika Tamasha la tatu la la Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10, 2011 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui Mkoani Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa kwa wakati huo Mh. Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila makuu katika Kanda ya Ziwa ambayo Wasukuma na Wanyamwezi wanaopatikana katika Mikoa ya Tabora, Shinyanga na Mwanza.
Akizunguma katika Mkutano na waandihi wa habari uliofanyika leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutano Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions Amon Mkoga alisema wasanii waliofanya vizuri mwaka huu ni Ali Mango , Asha Kaombwe, Hamisi Mpiga, Paulina Muhala na Paul Magadala.
Wsanii hao wataungana na wasanii wengine wa miaka miwili iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili itakayoitwa MWANAMILAMBO ambayo itakuwa ikipiga muziki wake katika asili ya makabila hayo na utakuwa muziki wa hotelini , maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.
Mkoga anazitaja nyimbo zitakazorekodiwa kuwa ni Kamnyangala Kane, Usoga wi kuwa, Kushoke Kukaya, Kana nabuta, Sensema Malunde, Ng'ombe Yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka 50 ya Uhuru.
Lengo kuu la kuanzishwa kwa bendi hiyo ni kusaidia kuhifadhi nyimbo mbalimbali za asili zilizotumiwa na wazee wa kale katika vita, kilimo,harusi na hata mazishi.
"Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho" anasema Mkoga.
Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika Studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John .a.k.a Nice P.
Pia kopi kadhaa zitatolewa latika vyuo, makumbumbusho ya taifa na mashuleni ili wanafunzi na wanvyuo waweze kuutambua utamaduni wao.
0 Comments