KAMPUNI MAMA YA BILICANAS GROUP WAPIGA JEKI , TAFRIJA YA SHEAR ITAKAYOFANYIKA OKTOBA MOSI 2011

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni  Mama ya Bilicanas Group  Dkt. Lilian Mtei Mbowe  yenye Kampuni Tanzu za Free Media Limited ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Aishi Protea Hotels, Club Bilicanas na Much More Club ,wakwanza kulia anaye onyesha mfano wa gazeti leo imetangaza litoa  udhamini mnono wa sh. mil 7.5 kwa Kampuni ya Shear Illusions ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya tafrija ya hisani ‘Shear Charity Ball’ iliyopangwa kufanyika Oktoka mosi mwaka huu katika hoteli ya Movenpick Jijini Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bilicanas Group Dk. Lilian Mbowe, katika mkutano wa pili wa Shear Charity Ball uliofanyika katika hoteli ya Peacock Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mbowe alisema mbali ya fedha hizo pia udhamini mwingine uliotolewa na Bilicanas Group katika tafrija hiyo ni pamoja na kutoa matangazo katika magazeti ya Tanzania Daima na Sayari katika siku maalum kadhalika wameandaa ‘After Party’ itakayofanyika Much More Club mara baada ya tafrija hiyo Oktoba Mosi.aliyekaa katikati ni Ofisa wa Mambo ya Ndani kutoka Kampuni ya Bia Serengeti ambao ndiyo wadhamini wakuu Imani Lwinga na Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni Shear Illusions Shekha Nasser.

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Shear Illusions Shekha Nasser alisema kundi la wacheza dansi wa muziki wa miondoko ya Salsa linalofahamika kwa jina la ‘Mutati Dancers’ toka nchini Kenya na Kundi la wasanii kutoka nyumba ya vipaji ya Tanzania House of Talent (THT) watapamba usiku wa tafrija hiyo ya hisani ya Shear.
Tafrija hii inafanyika kwa mara ya pili mfululizo ikiandaliwa na Kampuni ya Kampuni ya Shear Illusions ya hapa nchini yenye lengo la kutunisha mfuko na kusaidia kina mama wenye matatizo ya fistula katika hospitali ya CCBRT na pia kuwezesha ukarabati wa mfumo mzima wa maji safi na maji taka katika hospitali ya Amana zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Tafrija hiyo imepangwa kuanza saa moja usikI katika ukumbi wa Kivukoni, uliopo katika hoteli ya Movenpick. Ticketi zote za tafrija hii zitauzwa kabla ya siku ya tafrija.

Katika hafla ya mwaka jana kiasi cha sh.mil. 15 zilichangishwa huku nusu ya fedha hizo zilikwenda CCBRT kwa ajili ya matibabu ya akina mama wanaosumbuliwa na fistula wakati nusu ya fedha nyingine zilipelekwa kuwasaidia watoto wanaolelewa katika vituo vya SOS jijini Dar es Salaam.
Kutokana na ukubwa wa mahitaji, katika tafrija ya mwaka huu inalenga kuchangisha shilingi milioni 50 kwa ajili ya taasisi hizo mbili, za CCBRT na hospitali ya Amana zote za Mkoa wa Dar es salaam.

Shekha aliwashukuru wadhamini ambao wamejitolea kwa hali na mali katika kufanikisha tafrija hii ambao ni mdhamini mkuu Serengeti Breweries, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Billicanas Group, Kampuni ya kimataifa ya ulinzi ya Group 4, Shirika La Nyumba la Taifa (NHC) na Fly 540.
Wadhamini wengine ni Maxcom, Precision Air, Desktop Production (DTP), Peacock Hotel, Clouds Media Group, kampuni ya vifaa vya ujenzi ya SS Concrete, benki ya Azania, Benchmark Production, Advertising Dar, SBC Tanzania (Pepsi), Tanzania House of Talent (THT), I-View Media, mafuta ya kulainisha ngozi – Cocotan, duka la nguo la Tina Maria, Kampuni ya kupamba ya Hugo Domingo, Imaging Smart na AIESEC.

Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ulinzi ya 4Gas   ambao pia ni kati wadhamini wa tafrija hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Ursino Jacqui  Botha .

Post a Comment

0 Comments