Rais wa Zazibar Dk Alli Mohameed Shein akimsikiliza mwanafunzi wa Sekondari ya Waschana ya WAMA NAKAYAMA aliyekuwa akitoa maeleo mara baada ya , kuzinduliwa rasmi kwa shule hiyo.
Wasichana hawa ambao waliweza kudhihirirsha kwamba mtoto wa kike akipewa nafasi anaweza wote wanatoka katika familia zisizojiweza na yatima ambao wanasomeshwa na Taasisi ya WAMA.
Maelezo yakiendelea .
Nikiripoti kutoka Nyamisati ,Rufiji mimi ni Khadija Kalili.
RAIS wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ameipongeza taasisi ya wanawake na maendeleo WAMA katika kuboresha maendeleo ya mtoto wa kike hapa nchini.
Dk. Shein alitoa pongezi hizo juzi jioni wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati Wilayani Rufijii Mkoani Pwani.
Uzinduzi huo uliovunja rekodi kwa kuhudhuriwa na wake wa marais na viongozi waandamizi wakiwemo wake za Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi mama Khadija na Sitti Mwinyi, Mke wa Rais wa sasa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mwanamwema Shein ambaye pia ni Mjumbe Taasisi ya WAMA.
Dk Shein alisema mafanikio makubwa ya WAMA yanatakiwa kuigwa na taasisi nyingine.
“Taasisi zingine ziige, na nimefurahi kusikia wanafunzi wa hapa wanatoka Tanzania nzima ikiwemo Zanzibar kwani hata pale nilipokuwa katika ziara fupi nimekutana na wanafunzi kadhaa kutoka Zanzibar jambo la kuurahisha sana” alisema Shein.
Rais Shein aliongeza kuwa jukumu la kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumi ni la kwetu wote.
“Nachukua fursa hii kuipongeza tasisi ya WAMA Nakayama kwa kujenga shule hii ya wasichana yenye nchepuo wa Sayansi. Nina imani katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo kitabadilisha mawazo kwa watoto ambao hawakupewa elimu na kunyimwa fursa’ Alisema na kuongeza kuwa sasa ni wakati wa kuamka kwani watoto wote wana haki sawa ya kupata elimu sawa na mtoto wa kiume” alisema Shein.
Alisema hivi sasa uwiano wa kielimu kati ya mtoto wa kike na wa kiume unaridhisha na serikali inaweka mikakati ya kumuinua kielimu mtoto wa kike huku akisema malengo hayo kwa sasa yamewekwa katika udahili kwa vyuo vikuu.
Mwakilishi wa Balozi wa Japani ambao ndiyo waliotoa mchango mkubwa katika unjenzi wa shule hiyo Shuichiro Kawaguchi ametoa pongezi kubwa wa Taasisi ya WAMA kwa kuutumia vyema msaada kutoka nchini japani na amefurahi kuona shule hiyo ya wasichana iko katika mazingira mazuri na katikati ya vijiji
“Baada ya mama Salma Kikwete kutoa wazo la kujenga shule itakayowasaidia watoto wa kike kwa Nakayama ambaye ni Rais wa Kampuni kubwa duniani ya SAGA, aliamua kubeba gharama zote za ujenzi kwa kupitia taasisi ya WAMA hadi hapa tulipofika hivyo binafsi naona ni jambo la fahari leo kuwa mwakilishi wake na habari hizi nitazifikisha kama jinsi nilivyoona majengo na shule ya kisasa hapa Rufiji ” alisema Kawaguchi
Rais wa Zanzibar Dk. Alli Mohammed Shein mwenye siti ya buluu kulia kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake (WAMA) ambaye pia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakipata maeleo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMANAKAYAMA ,iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, Kibiti Rufiji Mkoani Pwani.
0 Comments