Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Ambilikile Mwasapila pichanai akitoa dawa.
Na Mwandishi Wetu
MWANDISHI mahiri wa vitabu, Atufigwege Mwakalinga ametunga kitabu cha maisha ya mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila.
Mwasapila maarufu kwa jina la ‘Babu la Loliondo’ anaishi kijiji cha Samunge mkoani Arusha, aliibuka miaka mitatu iliyopita na dawa inayoelezwa kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa matano sugu ambayo kwa kiasi kikubwa yamegharimu maisha ya Watanzania.
Chati yake ya dawa ya asili anayodai kuwa ameoteshwa na Mungu, ilipanda mapema mwaka huu kiasi cha kuvuatia watu wengi wakiwmao kutoka nje ya nchi hasa majirani wa Tanzania .
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi jijini Dar es Salaam na Mwakalinga inasema kwamba kitabu hicho kinachoitwa ‘Utamtambuaje Nabii’ kinaelezea huduma anayotoa kwa mafanikio makubwa huku ikisema “Kitabu hiki kimekamilika”.
Mwakalinga alisema amechukua hatua ya kuandika kitabu cha Babu wa Loliondo baada ya kumtembelea tabibu huyo na kushuhudia jinsi huduma yake inavyoendeshwa kwa mafanikio makubwa.
“Nina kibali cha Babu wa Loliondo kuandika kitabu kinachohusu huduma na historia ya maisha yake,” alisema Mwakalinga katika sehemu ya taarifa hiyo.
“Mchungaji Mwasapila amenipa ushirikiano mkubwa wa kuandika kitabu hiki kwani ni mambo mengi ambayo watu hawajapata kuyasikia na kujua juu ya huduma yake,” alisisitiza Mwakalinga.
Tiba hiyo mbali ya kufaidisha watu na kupata nafuu kutokana na mardahi, pia ilikomboa majirani wa Babu wa Loliondo ambao kwa biashara ndogondogo walivuna walichostahili, kadhalika Sarikali ilikusanya kodi kwa wenye magari na ndege.
Huduma hiyo ya Mch. Mwasapila pia imeinufaisha nchi ya Tanzania kupata fedha za kigeni, ingawa kwa sasa tatibu huyo anakabiliwa na vipingamizi kutoka kwa waganga wa kienyeji ambao wanakosa wateja.
“Wapinzani wengine ni madaktari ambao na wao wanahofia hospitali zao itafika wakati ambapo zitakosa wagonjwa, kwa sababu baadhi ya wagonjwa wanaolazwa mahospitalini wamethubutu kuondoka na magonjwa yao na kwenda kwa Babu kupata tiba,” alisema Mwakalinga.
Alisema kwamba katika kitabu chake amewataja wapinzani wengine wa Babu ni watu wenye imani kali za dini ambao hawaamini kwamba Mungu anaweza kumtumia Babu wa Loliondo, kwa visingizio kwamba si mlokole.
Mwakalinga ambaye katika kufanya kazi hiyo amedhaminiwa na Kampuni ya Biafra Travel Ltd, inayosafirisha abiria kwenda Loliondo kila wiki mara tatu, tayari amekisambaza kitabu hicho. Kitabu chake kingine alichotoa hivi karibuni ni ‘Pata Hekima, Pata Maarifa’.
0 Comments