Aliyekuwa Miss Tanzania 1999 na Mwandishi wa kitabu NAYAKUMBUKA YOTE Hoyce Temu akichangia mambo muhimu kuhusu kitabu chake katika tamasha la PEN & MIC lililofanyika katika mgahawa wa Saffron uliopo kwenye jengo la Quality Plaza.
Hoyce Temu akifafanua jambo kutoka katika nakala ya kitabu chake.
Mwandishi wa kitabu cha NAYAKUMBUKA YOTE Hoyce Temu akimkumbatia mfadhili wake mkuu Bwana Walter Bgoya kama ishara ya kumshukuru katika tamasha hilo.
Hoyce Temu akimkumbatia mke wa mfadhili wake mkuu Bi. Bgoya.
wandishi wa Kitabu Hoyce Temu akipongezana na rafiki ya mpenzi Hobokela Magale katika tamasha la PEN & MIC mara baada ya kutoa ufafanuzi wa kuwa mshauri wake mkuu.
Mrembo wa Tanzania 1999 Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Mrembo wa Tanzania 2002 Angela Damas.
Mwandishi wa Kitabu Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wake wa kazi kutoka UN Sala Patterson (kushoto) pamoja na mdau.
Msanii kughani mashairi Crystal Leigh Endsley ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama wa tamasha la PEN & MIC akionyesha umahiri katika fani hiyo.
Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya MKUKI na NYOTA ambayo ndiyo imechapisha kitabu cha Hoyce Temu. Kitabu NAYAKUMBUKA YOTE kiko mitaani tayari na kinapatikana kwa shilingi 5000 kwa nakala lengo likiwa ni kuhamasisha wasichana na wanawake wanaopitia magumu katika maisha.
Wadau wakishangilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya watu na wadau mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo.
Rais Samia anawajali watu wenye Mahitaji Maalum: Naibu Waziri Mwanaidi
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Tanzania Mhe Mwanaidi Ali Khamis akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa
Nyumba ...
8 hours ago
0 Comments