MTAMBUE MCHORAJI WA KIMATAIFA MZEE RAZA

Mohamed Raza kulia  pichani akiwa na Frank wa URBAN PUSLE  ni Msanii Maarufu wa kimataifa ambaye ni hazina Halisi ya Taifu letu la Tanzania, alianza kazi yake ya  sanaa za kuchora tokea enzi za Uhuru wa Tanganyika. Vizazi zaidi ya viwili vimenufanika na kuelimika kwa kusoma vitabu vyake tokea shule za msingi mpaka secondary hasa vya kiingereza kama familia ya Mr & Mrs Daudi na Mtakuja Primary School. Mbali na hapo Mzee Raza aliwahi kumchora Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Miaka ya 1960 na kufanikiwa kupata kazi katika chama cha TANU. Pia aliwahi kufaya kazi katika ubalozi wa Marekani Hapa Tanzania miaka ya 70.Orodha haikuishia hapo aliendelea kuchora na kudesign stempu pamoja na nishani za mashujaa wa vita vya Kagera pamoja na kuwachora viongozi wengine wa serikali.
URBAN PULSE Ikishirikiana na Mwandishi Nguli wa habari Freddy Macha wanakuletea programme maalum ya Mzee Raza walipopata bahati ya kukutana nae  hapa jijini London na kumdadisi kwa undani katika safari yake ya sanaa za michoro pamoja na changamoto mbalimbali zinazomkabili. Wakati Tunaelekea katika Miaka 50 ya uhuru hatuna budi kukumbuka, kutambua na kumpatia heshima yake anayostahili  kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika jamii yetu na ambaye ni Hazina ya taifa letu.ogramme hii itakuwa katika sehemu tatu, hivyo basi juinge nasi ili upate kumfahamu Mzee Raza kwa ukaribu zaidi,
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE

Post a Comment

0 Comments