MARHABA YA SHAHARU RAMADHAN -WAISLAMU WA MJI WA READING WAFTURU

Baadhi ya Viongozi wa REACO wakiwa katika picha ya pamoja.
 Salam Alleykum,
READING EASTERN AFRICAN COMMUNITY(REACO) Iliandaa futari maalum leo jioni 28.8.11 na kuwaalika wanajumuia mbalimbali kutoka Reading, London, Coventry na sehemu nyingine ili kupata futari kwa pamoja. Hii ni desturi ambayo hufanyika kila mwaka wakati huu wa mwezi mtukufu ramadhani. Lengu kuu haswa ni kujumuika pamoja katika kudumisha upendo, amani na umoja kwa wana jumuia pamoja,kuzingatia yale yote yalio mema na kukataza yalio Mabaya.Mgeni Rasmi wa siku ya leo alikuwa Mh Naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na baadhi ya maofisa wa ubalozi wetu wa Tanzania Hapa London.Kwa niaba ya Mwenyekiti wa REACO Said Mahmud tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioitikia mwito na kuja kujiunga nasi. Tunawashuru sana.Kwa maelezo au mawasiliano zaidi tafadhali tutumie email ifuatayo, reaco@hotmail.co.ukAsanteni,URBAN  PULSE CREATIVE

 Baadhi ya viongozi wa REACO wakipata  futari.
 Mheshimiwa Chabaka akifurahia jambo wakati Afisa wa Ubalozi Kiondo akiteta na Ustadhi Sungura.
 Mheshimiwa Naibu Chabaka akiwa katika picha ya pamoja.
 Picha ya pamoja na wanajumuia
 Wanajumuiya wakipata futari pamoja na wageni waalikwa..
 Wanajumuia wakijiandaa kwa furati.
Watoto wakipata futari.

Post a Comment

0 Comments