NURUEL MBOWE AACHIA NGOMA MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA 'NYUMBANI'


Mwanamuziki mkongwe kwenye anga la bongo fleva anayekwenda kwa jina la Nuruel Mbowe ameachia wimbo mpya unaokwnda kwa jina la “Nyumbani”.Nuruel aliyetamba na nyimbo za mng’ao wa silva,chondechonde,umetutoka baba na nyimbo ya nzela aliyoshirikiana na B band kama jirani kwa sasa ameamua kuja na ujio mpya kwa watanzania.Nuruel alisema  baada ya kimya cha muda mrefu ,ameamua kurudi katika la burudani ili kuwapa raha mashabiki wake ambao walizikosa kwa muda mrefu.“Kiukweli nilikuwa kimya kwa muda mrefu na ninadhani huu ni muda muafaka kwa wapenzi wangu kupata kitu roho inapenda kwani kwa sasa nina wimbo wangu mpya uitwao Nyumbani nilioufanya studio za Fish crab”alisema Nuruel.Nuruel alisema kwa sasa yupo kambini na band yake mpya ambayo hakupenda kuitaja jina lake lakini aliwahakikishia watanzania kupata nyimbo zenye burudani sambamba na elimu pia.
“Kwasasa nipo kambini na band yangu mpya  ambayo sitopenda kuitaja kwasasa lakini inawanauziki wakali na wazuri”alisema Nuruel.Alisema matarajio yake hapo baadaye ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa pamoja na kufungua studio ya kurekodi nyimbo pamoja na kuwasaidia wanamuziki chipukizi.
“Matarajio yangu ni kuwa mwanamuziki nitakayetamulika kimataifa na kufungua studio ya kurekodi nyimbo”alisema Nuruel

Post a Comment

0 Comments