Mamia ya wakaazi wa Mkoa wa Iringa ambao walijitokeza katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika kwenye uwanja wa Samora.
Wasanii wakongwe wakonga wakazi wa Iringa ni katika Serengeti Fiesta
Na Mwandishi wetu , Iringa
WASANII wakongwe ambao walitamba katika miaka ya nyuma Inspekta Haroun, Profesa Jay, Mwana Fa juzi jioni waling’ara katika jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika kweny uwanja wa Samora mjini hapa.
Kukubalika kwa wasanii hao na kutochuja katika vichwa vya mahsbiki wa rika mbalimbali waliotumbuiza kwenye tamasha hili lilidhihirika pale Haroun ‘Babu’ alipopanda jukwaani na kuachia wimbo wa ‘Mtoto wa Geti kali’ na nyimbo zake kadhaa za zamani ambapo mayowe na kelele zilisikika huku wakimfuatisha kuimba.
Akiwa jukwaani alitambulishwa atapanda kama kundi la gangwe Mob hivyo kundi hilo likiongozwa na Inspekta lilikonga nyoyo ipasavyo.
Msanii mwingine ambaye mkongwe katika muziki wa kizazi kipya aliyeonekana kupokewa vyema na wakaazi wa mji wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ni Profesa Jay wa Mitulinga nay eye hakupata taabu kwani alipotangazwa na mshereheshaji kuwa ni zamu yake kupanda jukwaani watu walipagawa na kwenda naye sambamba katika kuimba nyimbo zake zote ikiwemo Zali la Mentali.
Amshaamsha ilikuja kwa Msanii Chid Benz ambaye alitia fora kwani ulipofika wakati wake palikuwa hapatoshi alishangiliwa na kila shabiki uwanjani pale huku wakirukaruka huku na kule yote hiyo ikiwa ni katika kusherehekea msimu wa dhahabu uanoendelea.
Wasanii wengine walioonekana kung’ara ni pamoja na Bob Junior , Godzilla, Joh Makini,Dayna, Rachel na kundi la Tip Top Connectin bila kumsahau 20% .
Tamasha hili limeratibiwa na Kampuni ya Prime Time Promotions kwa ushirikiano na Clouds Media Group huku mdhamini mkuu ni Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Serengeti Fiesta 2011 tayari imeshafanyika katika mikoa ya nMwanza ambako ndiko lilikoanzia huku msanii wa Kimataifa Shaggy akilipamba kwa aina yake.
Mikoa mingine ambako tayari Serengeti Fiesta 2011 imeshafanyika ni pamoja na , Dodoma, Shinyanga, Morogoro, Musoma na leo litafanyika kwenye uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya.
Godzilla mtoto wa Salala, akimwaga mistari jukwaani .

Profesa Jay moja kati ya wasanii wakongwe waliotumbuiza ambapo waling'ara huku mashabiki waliimba pamoja nayeye kama Zali la Mentali na nyinginezo.
Watoto wa Manzese Kundi la Tip Top wakiwa jukwaani katika tamasha linaloendelea la Serengeti Fiesta 2011.
20% akiwa Jukwaaani hapa akiwa mbaali ambapo amefanikiwa kwwa kuwapa msimu wa dhahabu wakazi wa Iringa kutokana na kuimba nyimbo zake zinazopendwa na wengi kama Tamaa Mbaya na nyinginezo.
Msanii wa kike anayechipukia Dayna akiwa jukwaaani katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Mkongwe Mwana Fa aling'ara huku wakazi wa Iringa wakionekana kushangilia nzaidi ngoma za zamani kweliu ya kale dhahabu.
Bob Junior aliamshaamsha ipasavyo wakati alipokuwa jukwaaani, na kuwachezesha wakaazi wa Iringa.
Kutoka kushoto ni mimi Khadija, Harieth mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Dennis Mlowe Mtangazaji wa Country Radio FM ya hapa Iringa, Mwanamuziki Profesa Jay na Godzilla hapa tukiisikilizia baridi ya Iringa inapuliza ile mbayaaa.
Mohammed Zimbwe Top C , akitoa shangwe katika Tamasha hilo na kubamba na kibao chake cha Nilipe Nisepe ambapo alishangiliwa ile mbayaaa.
Mohammed Zimbwe Top C , akitoa shangwe katika Tamasha hilo na kubamba na kibao chake cha Nilipe Nisepe ambapo alishangiliwa ile mbayaaa.
Kushoto ni msanii wa kike anayekuja juu Mwanaidi Nyange 'Dayna' na mimi tukifanya mahojiano mara tu aliposhuka jukwaani, Dayna anasema kwakuwa bado ni mchanga katika fani ya muziki yuko tayari kijufunza kutoka kwa wenzake pia anamalengo ya kuja kuwa mwanamuziki nyota katika ukanda wa Afrika Mashariki huku akitumanini kamba akiweza kupenya katikaukanda huo moja kwa moja ataweza kufahamika nje ya mipaka.Pia amewaomba radhi mashabiki wake kwa kupata ujumbe wenye maneno mazito kwa kupitia mtandao wa Facebook ambapo kuna mtu ameiba neno lale la siri PASSWORD halafu akawa anaandika maneno yenye kuchefua ambapo katika hali ya kawauida mtu hawezi kumwambia mpenziwake.
"Dada kuna mtu kaiba neno langu la siri la kuingia katika Acccount yangu kisha akawa anatuma meseji chafu za mapenzi huku akijifanya kuwa ni mimi,nimesikitika sana na nawaomba radhi wote kwa usumbufu walioupata hivi sasa nimebadilisha hivyo hawezi tena kuingia, yaani maneno aliyokuwa nayaandika huwezi amnini ameandika hivi......., (Akaninong'oneza mitusi yote na mimi siwezi kuyaandika ni mazito Looh), "katika hali ya kawaida hata kama mpenzi wako mmezoeana kiasi gani huwezi kumwambia hivyo anamalizia Dayna.
JAMANI HEBU TUBADILIKE JAPO KIDOGO MBONA TUNAPENDA KUCHAFUANA? HUYU DAYNA BADO NI BINTI MDOGO ANAYEANZA KUTAFUTA MAISHA YAKE WATU TUNAANZA MATIMBWILI BINAFSI NAWACHUKIA WATU AMBAO WANAPENDA KUWAKWWAZA WENZAO NA HAO WAMEFILISIKA KIFIKRA KATIKA MAISHA YAO HIVI KUMTUSI MTU AU KUMCHAFULIA MTU KWWA WATU WAKE INAWASAIDIA NINI ACHENI HIZOOO WABONGO SISI NDIYO WACHAWI WA MAISHA YETU KWANINI HAMPENDI KUONA MWENZENU ANASEMA NA NJAA ZAKE MNATAKA AJE AWAOMBE NYIE WAKATI NJAA ZENU MASHINDWA KUSEMA NAZO.DAYNA AMENIONYESHA MESEJI NI CHAFU KULIKO NA HUYU MTU ATAKUWA ANAMJUA KWA SABABU ANAYEKUTUKANA AU KUKUFANYIA UBAYA SIKU ZOTE NI MTU UNAYEFAHAMIANA NAYE ANAWEZA KUWA SHOGA YAKO, NDUGUYAKO, NA WENGINE NI WALE WENYE VISOKOROKWINYO VINAVYOWASUMBUA TU MIOYONI MWAO MWACHENI MTOTO WA WATU ATAFUTE ANDAZI,MUHOGO, KIAZI AU KITUMBUA CHAKE CHA KILA SIKU AU HAMPENDI KUMWONA ANANG'ARA TUNAJUA UREMBO WAKE NDIYO UNAOWAKWAZA WENGINE KUMBUKENI KILA MTU NA MAISHA YAKE NA JINSI ANAVYOJIWEKA KAMA ANAJISHAUA NA WEWE SI UTAFUTE UWANJA WAKO UKAJISHAUE KIVYAKO MATUSI NA KEJELI YA NINI.NIMEGUSWA NA HILI LILILOMKUT DAYNA HAIPENDEZI.
Bob Junior akiwa Jukwaani ambapo alikimbiza hadi watu wakasahau baridi kwa muda.
Mtangazaji wa Redio Clouds kupitia kipindi cha XXL B12 kulia akiwa na mshkaji wake kwenye Uwanja wa Samora Iringa.
Kutoka kushoto ni Harieth Makweta, Khadija na Danis Mlowe Mtangazaji wa Radio Country FM ya Iringa.
0 Comments