SERENGETI WAVUNJA REKODI MWANAMICHEZO BORA 2010, KUONDOKA NA ZAWADI YA GARI











MSHINDI wa Tuzo za mwanamichezo bora 2010 atazawadiwa zawadi ya gari aina ya GX100 litakalotolewa na mdhamini mkuu Kampuni ya Bia Serengeti.

Zawadi hiyo ilitangazwa leo katika mkutano na waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mahusiano Kampuni ya Serengeti Teddy Hollo Mapunda.

Gari hiyo yenye thamani ya sh. Mil 13 atakabidhiwa mshindi huyo siku ya tukio ambapo ni Mei 6, mwaka huu katika hafla iliyopangwa kufanyika katika hoteli ya Royal Palm Movenpick Dar es Salaam.

Juma ya wanamichezo 19 kutoka katika michezo ya aina mbalimbali wanatarajiwa kuania gari hilo ambapo itakuwa ni mara ya kwanza katika historia utoaji tunzo mshindi kupata zawadi nono kama hiyo.

“Sisi Serengeti tumeamua kufanya mageuzi na kuwathamini wanamichezo kwa ujumla kutokana na mchango wao katika kuitangaza nchi kwa kupitia michezo mbalimbali” alisema Teddy.

Aidha kila zaidi ya wanamichezo 30 kutoka katika michezo mbalimbali kwa upande wa wanawake na wanaume watapata zawadi ya kitita cha sh .mil 1 kutoka SBL.

Naye Mwenyekiti wa TASWA , Juma Pinto alisema kuwa kutakuwa na tunzo ya heshima kwa mwanamichezo anayefanya vizuri nje ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya tunzo hizo Massoud Sanani alisema mchakato unaendelea vizuri pia ametoa shukrani kwa TASWA kutokana na kuamua kuwashirikisha baadhi ya wanachama wake katika kuendesha gurudumu na hilo na kwa maendeleo ya TASWA kwa ujumla.

Wakati huohuo Teddy alisema Hoteli ya Movenpick wametoa ofa kwa mshindi ya kulala usiku mmoja katika hoteli hiyo yeye na mwenza wake.

Post a Comment

0 Comments