Meneja wa TP Mazembe Tzediric Kitenge(Mwenye T-Shirt), anayefuata ni Jean Dieu na Kocha wa Simba Patric Phiri , wakizungumza na wanahabari leo mchana katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kutoka kushoto ni , Mgosi, Phiri na Tzedic. Pichani Kocha wa Simba Phiri akizunguimza na wanahabari leo TFF ikiwa ni siku moja kabla ya mechi. Na Dina Ismail Wakati kesho zinashuka kwenye dimba la Taifa kukwaana katika mechi ya marudiano ya ligi ya klabu bingwa ya Afrika timu za Simba na Tp Mazembe kila mmoja imejitapa kutoka kifua mbele. Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), viongozi wa timu hizo kila mmoja aliahidi timu yake kutoka kifua mbele. Kocha mkuu wa Simba Mzambia Patrick Phiri alisema kwamba amekiandaa vema kikosi chake na hasa kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi ya awali hivyo ana uhakika watatoa kifua mbele. Alisema anajisikia fahari kucheza na vinara wa soka mara mbili mfululizo barani Afrika lakini hilo haliwatii hofu wachezaji wake kucheza vema na hatimaye kushinda mechi hiyo. “Mazembe ni kama walimu soka Afrika, wamekuja kutufunza soka...lakini hiyo si sababu ya kutufanya tupoteze mechi yetu, naamini tutashinda na kuweka historia”, Alisema Phiri. Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri ya mchezo huo ambao kwa namna moja au nyingine ni lazima washinde ili kusonga mbele. Naye Meneja wa Tp Mazembe Tzediric Kitenge alisema kuwa wamekuja na kikosi cha maangamizi hivyo ni lazima waibuke na ushindi. Alisema bao pekee walilolipata Simba katika mechi yao ya awali iliyochzwa katika jiji la Lubumbashi si kigezo kuwa wataweza kuwafunga mabao zaidi na kuwatoa katika michuano hiyo. Katika hatua nyingine, Kitenge alikana timu yao kutoa rushwa kwa waamuzi katika mechi yao ya awali na Simba na kusema kuwa tuhuma hizo zina lengo la kuwaharibia. “Kama kuna kitu hicho mtu aje na kuthibitisha, timu yetu nzuri na imewahi kuzifunga mabao mengi timu kubwa ikiwemo Esperance (Tunisia) na nyinginezo, hiyo ni katika kupakana matope”, Alisema. Naye mshambuliajui wa Simba Mussa Mgosi alisema wapo vizuri kimchezo na leo lazima historia ya mwaka 2003 ijirudie. MO ATANGAZA DAU LA MILIONI 50 ENDAPO SIMBA WATAICHABANGA TP MAZEMBE Na Dina Ismail Wakati kesho zinashuka kwenye dimba la Taifa kukwaana katika mechi ya marudiano ya ligi ya klabu bingwa ya Afrika timu za Simba na Tp Mazembe kila mmoja imejitapa kutoka kifua mbele. Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), viongozi wa timu hizo kila mmoja aliahidi timu yake kutoka kifua mbele. Kocha mkuu wa Simba Mzambia Patrick Phiri alisema kwamba amekiandaa vema kikosi chake na hasa kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi ya awali hivyo ana uhakika watatoa kifua mbele. Alisema anajisikia fahari kucheza na vinara wa soka mara mbili mfululizo barani Afrika lakini hilo haliwatii hofu wachezaji wake kucheza vema na hatimaye kushinda mechi hiyo. “Mazembe ni kama walimu soka Afrika, wamekuja kutufunza soka...lakini hiyo si sababu ya kutufanya tupoteze mechi yetu, naamini tutashinda na kuweka historia”, Alisema Phiri. Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri ya mchezo huo ambao kwa namna moja au nyingine ni lazima washinde ili kusonga mbele. Naye Meneja wa Tp Mazembe Tzediric Kitenge alisema kuwa wamekuja na kikosi cha maangamizi hivyo ni lazima waibuke na ushindi. Alisema bao pekee walilolipata Simba katika mechi yao ya awali iliyochzwa katika jiji la Lubumbashi si kigezo kuwa wataweza kuwafunga mabao zaidi na kuwatoa katika michuano hiyo. Katika hatua nyingine, Kitenge alikana timu yao kutoa rushwa kwa waamuzi katika mechi yao ya awali na Simba na kusema kuwa tuhuma hizo zina lengo la kuwaharibia. “Kama kuna kitu hicho mtu aje na kuthibitisha, timu yetu nzuri na imewahi kuzifunga mabao mengi timu kubwa ikiwemo Esperance (Tunisia) na nyinginezo, hiyo ni katika kupakana matope”, Alisema. Naye mshambuliajui wa Simba Mussa Mgosi alisema wapo vizuri kimchezo na leo lazima historia ya mwaka 2003 ijirudie.
Uchaguzi : INEC yawanoa Ma-OCD nchini kuhusu sheria za uchaguzi
-
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima
Ramadhani akizungumza jambo wakati wa mafunzo kuhusu sheria za uchaguzi kwa
Makama...
31 minutes ago
0 Comments