Timu ya TP Mazemba kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasi-DRC, imewasili jana jioni jijini Dar es Salaam, tayari kwa mtanange wao unaotarajiwa kuwa mkali dhidi yao na Simba ya hapa, katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa kesho Aprili 3 . Kikosi na viongozi wa timu hiyo waliwasili mida ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Mechi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kwa mashabiki kwa kuwa Simba inahitaji kushinda mabao 2-0, kwani katika mechi ya awali iliyopigwa Lubumbashi Machi 20, Simba ilikwanyuliwa mabao 3-1.Timu ya TP Mazembe wameingia na mkala wa kuja na mashabiki wale 600 ambao watataoa hamasa kwa timu hiyo.Wakati huohuo Watanzania wametakiwa kuweka uzalendo mbele na wote kutoa sapoti kwa kuishangilia timu ya Simba.Hiyo imekuja baada ya kubainika kwamba mashabiki wa Yanga wamejipanga kuishangilia TP Mazembe kwa nguvu zote ikiwa ni katika kulipiza kisasi kwa Simba ambao walijiunga n mashabiki wa El Ahly na kuwapa sapoti waaarabu hao walipo cheza na Yanga.
WATU WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI MADAI YA KUHARIBU,KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA
RELI YA KISASA (SGR)
-
WATUHUMIWA Watano Wakiwemo Raia Wa China Wawili Wanaokabiliwa na Tuhuma
za Kuharibu Miundombinu Ya Reli Ya Kisasa (SGR) Wamepandishwa Kwa Mara
ya p...
7 hours ago
0 Comments