Kushoto ni Mwakilishi wa BASATA Omari Mayanga na Lundenga.
MAWAKALA ambao huandaa mashindano ya urembo ,Miss Tanzania leo wametoa dukuduku lao kwa Kamati ya Miss Tanzania na kuomba waandae kanuni zitakazowabana warembo watakaotwaa taji la Taifa yaani Miss Tanzania pindi watakapofanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
Mawakala hao ambao wamesema hayo leo katika semina ya siku moja iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo.
“Mkurugenzi Lundenga tumekuwa tukipata wakati mgumu wa kupata warembo wenye vigezo kwani wengi wazazi wao hukataa kuwata ruhusa ya kushiriki kutokana na vitendo wanavyovifanya warembo waliokwisha pata mataji na hasa Miss Tanzania” alisema wakala mmojawapo.
Akijibu hoja hiyo kwa kifupi Mkurugenzi pia Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akajibu kwa kusema kwamba wao hawastahili kupewa lawama hizo na jamii kwa kila mshiriki anayekuja na kuingia kambini huwa ana malezi yake huko alikotoka yaani kwa wazazi wake au walezi, lakini katika kuchukua tahadhari watakaa na kuweka mkakati wa kukabiliana na na tatizo hilo huku akiwataka wakala wote washirikiane na Kamati ya Miss Tanzania ili kuweka nidhamu ya mashindano hayo.

0 Comments