Maonyesho ya Harusi yaliosubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wa masuala ya harusi na watarajiwa wa harusi yameanza leo katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE huku yakiwa na washiriki zaidi ya 51 waliochukua mabanda kwa kuonyesha na kuuza biashara zao. Wakizungumza kkwa nyakati tofauti tofauti washiriki hao ambao wamejitokeza kwa wingi, waliyasifu maonyesho ya mwaka huu na kusema kuwa yamekuwa hai na mvuto wa aina yake, kwa kuwa mambo mengi yameongezeka kwa mwaka huu. "tulishiriki mwaka jana, na mwaka huu pia, ila mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi na yenye kupangiliwa zaidi, kwa kweli waandaaji wamejipanga vilivyo" alisema mmoja wa washiriki toka kampuni ya picha ya GRM. Maonyesho ya mwaka huu yameongezewa ladha kwa kuongezewa vitu mbaliombali, ambapo mbali na kuongezeka kwa nafasi na mabanda, pia kuna upya wa vitu kama 'mdahalo wa Harusi' ambapo wataalamu waliobobea katika masuala ya harusi watazungumza na wale watakaotembelea maonyesho hayo. Huku jarida la kwanza na la aina yake la kitanzania 'HARUSI MAGAZINE' chini ya usimamizi wa mbunifu wa mavazi maarufu nchini Mustafa Hassanali likisambazwa ukumbini hapo kwa toleo lake la kwanza. Wadau wote na wakaazi wa jiji la Dar ess salaam wanakaribishwa sana katika maonyesho haya ya siku tatu yanayoendelea ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee. Mfaume Shaban Media & PR Manager Mustafa Hassanali PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania 105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania (opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy) Tel : +255 (0)22 266 8555 Mobile : +255 (0)655 501 526 Mail : media@mustafahassanali.net Web : www.mustafahassanali.nethttp://www.swahilifashionweek.com/
MWANAMKE MMOJA AFARIKI DUNIA AJALI YA ROLI MBEZI KWA MSUGULI
-
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya gari aina ya roli lenye namba ya
usajili T696 CLY kuacha njia na kumgonga mwanamke ...
6 hours ago
0 Comments