Na Janet Josiah
Kufuatia mapigano makali ya ardhi kati ya wananchi zaidi ya 400 na mabaunsa 160 yaliyotokea katika kijiji cha Nakalekwa- Tegeta Wilayani Kinondoni, watu 17 wakiwamo Viongozi wa Serikali za Mtaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Nchini.Viongozi wanaoshikiriwa ni pamoja na wale wa serikali za mitaa ya Mivumoni na Madale Pichani
Kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela.
wananchi wanaojiita waereketwa wa uvamizi wa eneo hilo ambao waliwahamasisha wananchi kuchukua silaha za jadi kama mapanga, visu na mishale kuwashambulia mabaunsa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela, alisema viongozi na wananchi hao, saba wamekamatwa kwa tuhuma za kosa la mauaji na tisa wanatuhumiwa kwa kosa la kuharibu mali ( nyumba tano za wakazi hao. Kamanda Kenyela alisema kutokana na makosa yenyewe yalivyo, majina ya watuhumiwa wa makosa hayo yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi na kwamba pindi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.
Aidha Kamanda Kenyela alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa tukio hilo la mauaji liliandaliwa kutokana na viongozi na wanachi hao kujipanga na silaha katika barabara ambazo mabaunsa hao walizitumia kupita ili kujiokoa.
Aidha Kamanda Kenyela aliwataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwezesha watuhumiwa zaidi walioshiriki matukio hayo waweze kukamatwa. Alitoa Rai kwa wananchi wa eneo hilo na kuacha kutoa taarifa na kauli zenye ushabiki wa kupotosha ukweli wa tukio hilo ambalo alisema linaweza kupandikiza chuki miongoni mwa jamii na kusababisha baadhi yao wakose imani na jeshi lao.
Katika mapigano hayo yaliyotokea April 7 mwaka huu, watu wawili kati ya mabaunsa 160 ambao ni Godfrey Samwel maarufu kama Kabigi na Hatibu Hemed maarufu kama Double Diff waliuwawa baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi wenye hasira kali.
Mabaunsa hao walikuwa wakiendelea na operesheni ya kubomoa nyumba za wakazi wa Mtaa wa Madale wa Kijiji cha Nakalekwa wilayani humo kwa amri ya Daniel Chacha (39), mkazi wa Mikocheni 'B', ambaye anadai ndiye mmiliki halali wa eneo la ekari zaidi ya 104.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kenyela alisema Jeshi la Polisi wilayani humo limeyakamata magari 230 zikiwamo daladala 126 na magari mengine 104 kwa makosa mbalimbali.
Alisema magari hayo kwa pamoja yalifanya jumla ya makosa 482 katika operesheni ya kuzui uhalifu wa makosa ya usalama barababani ambayo yalitozwa faini ya tozo la ‘notification’ na kupatikanana kiasi cha zaidi ya shilingi milioni tisa.
Na katika tukio jingine lililotokea usiku wa kuamkia jana, Jeshi hilo lilikamata magunia matatno ya bangi yenye kilo 90, katika maeneo ya Boko Dovya, yakiwa yamebebwa katika gari lenye namba za usajili T.513 BQB aina ya Toyota Corolla.
0 Comments