Habari zilizo tumwa na mdau muda huu zinasema huko jijini Mwanza katika maeneo haya Kikubiji Wilayani Kwimba , Geita Magu sasa nako wameibuka watu nwengine wakidai wameotesha na wanatoa dozi ya kikombe kinachotibu magonjwa sugu ikiwemo UKIMWI huku misururu ya watu wanaofuata tiba hiyo ikizidi kadri muda unavyozidi .Dawa hizo zimechukuliwa kupimwa kama hazina madhara kwa mtumiaji huku Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akisubiriwa kutoa tamko.Huku baadhi ya wadau wakishauri watu kutokimbilia kunywa vikombe bila kupima kisayansi kama wameathirika au vinginevyo licha ya kwamba hilo ni suala la kiimani zadi.Wengi wanaona ni neema imewashukia.Angalizo waliokunywa kikombe wanatakiwa kupima baada ya miezi mitatu.Nakubali mtu anapoumwa kwa muda mrefu huwa anakata tamaa hivyo kuwa tayari kujitibu kwa njia yoyote ile hasa njia fupi kama ya kikombe.
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
5 hours ago
0 Comments