ashkaji mambo vipi ,leo msomaji wangu nitawadadavua wale wenye kulisukuma gurudumu la tasnia ya Filamu nchini inayokuwa kwa kasi, ambapo pia nimekuletea mada motomoto ya ‘Behind the seen’ au waweza sema nyuma yaliyojiri ,nyuma ya pazia na vinginevyo.
Sasa ni hivi jamani neno hili la nyuma ya pazia ambalo limeanza kuota mizizi kwa wanasanaa hasa wa filamu za hapa nchini kwetu hasa wanaporekodi filamu zao ambapo wamekua walikitumia ndivyo sivyo.
Hakika kila mdau wa filamu atakuwa ni shahidi katika hili ambapo utaona mara baada ya filamu inapo malizika unaona yanakuja mambo mengine ambayo hata hayaeleweki.
Hivi huu ni uungwana kweli jamani? au tunakuwa tunatumia filamu kutaka kuonyesha majaaliwa ya miili na jinsi tulivyoumbwa au? kama hiyo haitoshi utaona na kusikiwa maeneo ambayo hayastahili kusikia pamoja na vitendo visivyostahili kuonekana hadharani hasa kwa wanawake, huku wengine wakikata mauno ambapo lengo ni kuonyesha jinsi walivyo na viuno vilaini au vinginevyo hayo wanayajua wenyewe.
Mifano ya ‘Behind the seen’ iko kwenye filamu nyingi hapa kwetu ila sitopenda kuzitaja majina kwa sababu ya kutotaka kupotezea biashara za watu lakini katika filamu zijazo nawashauri wasanii kutupilia mbali mambo ya nyuma ya pazia kwani mengi hichakachua filamu husika na kupoteza maana na kutupilia mbali hisia alizopata mtazamaji.
Kadhalika sitopenda kutaja majina ya wasanii ambao wamekuwa vinara wa kukata mauno na kuvaa mavazi yasiyofaa huku wakionyesha miili yao kwenye filamu hizo kwa sababu wenye shepu nzuri na miguu mizuri ya kuvalia nguo fupi huwa wala hawana mishebeduo ya namna hiyo na pale siyo mahali pake.
Ni kweli mtu ukitaka kwenda na mitindo inayobamba hupaswi kujiangalia umeumbwa vipi au ukoje huko mimi siko ila katika suala la kusoma alama za nyakati imo bwana siyo unakurupuka tu na kuvaa mavazi ambayo hata wewe mwenyewe unaona dhahiri kwamba hauko huru kabisa.
Laiti kama wasanii wetu wangeng’amua kwamba wao ni kioo cha jamii wasingekuwa wakifanya mambo kama hayo ambayo hayana nafasi ya kuleta tija yoyote katika tasnia babkubwa ya filamu ambayo imeshika chati kwa sasa na kuweza kutoa ajira binafsi kwa wasanii wanaoibuka kila kunapokucha.
Wakati umefika kwa wasanii wetu wawe wanaandaliwa japo kwa kupata semina fupi fupi pamoja na mafunzo mbalimbali ambayo yatakuwa yakiwafunza mipaka yao katika kazi na pamoja na kupata misingi bora ya kuwa msanii.
Nasema hivyo kutokana na uhalisia ambao uko wazi hivi sasa ikionekana huyu dada au binti ana mvuto basi hapo kapeta kuigiza katika filamu, hapo Madairekta mapotoka.
Hapo sasa ndipo ninapo jiuliza, hivi wadau na wakufunzi wa masuala Tasnia ya filamu nchini wako wapi na wanafanya nini katika kuinusuru fani yao kama siyo kuiendeleza.
Lakini wakati nikiwa najiuliza kuhussu jambo hilo ndipo mwishoni mwa wiki nikiwa nimejipumzisha nyumbani kwangu na macho yakiwa yametulia katika luninga ndipo nikatua katika stesheni moja na kukutana na kipindi cha Bongo Movie, hapo nikakutana na mtangazaji Yvone Cherry almaarufu kwa jina la ‘Monalisa’,ambaye fani yake ni mwigizaji aliyeanza kung’ara katika fani hiyo akiwa na kundi la Nyota Ensemble huku akiwa na waigizaji nyota kina Ray, Richie, Bisahanga, Waridi na wengineo.Siku hiyo Yvone alikuwa na mada ya kuhusu hilo gonjwa la ‘Behind the seen’, naam nami nikaona acha niwasikie wenye fani yao ili na mimi nipate la kuwaandikia katika safu yangu ya Busati ambyo huchapishwa kila siku ya Ijumaa kwenye Gzeti la Tanzania Daima.
Alianza Muongozaji galacha wa filamu nchini George Tyson yeye alipinga na kusema wazi kwamba anakerwa sana kuona wasanii wamekuwa wakijidhalilisha na kwa wanaojua maana ya neno hilo la ‘Behind the seen’ linavyotumika ndivyo sivyo kwenye tasnia hiyo na wasanii wa filamu nchini ni aibu kubwa.
Wakati nikikaa sawa kumsikiliza Tyson aliendelea kwa kusema kuwa “Behind the seen hutumikaa katika kuonyesha baaadhi ya vipande vyenye kuvutia wakati filamu ilipokuwa ikiandaliwa na kuonyesha mapito magumu au vinginevyo wakati filamu hiyo ikiandaliwa lakini sivyo inavyoonekana hivi sasa huu ni utoto wasanii waache, utaona mtu anafanya vituko vya kihuni kama kukata mauno na kuvaa nguo zisizostahili huku wengine wakionekana kucheza muziki wa Aladji haipendezi binafsi inanichefua kwa kweli” alisema Tyson.
Naye Mkufunzi wa masuala ya filamu Ndunguru alitoa maoni yake huku akikemea vikali jinsi wasanii wa filamu wanavyo potosha umma na kuhusu matumizi ya ‘Behind The Seen’.
Ndunguru amewataka wasanii kutojidhalilisha kitaaluma kwa kuonyesha jinsi walivyo mahiri kwa kupigana mabusu na kuonyesha mambo ambayo hayapendezi kwani wanapaswa wakumbuke kuwa kazi zao zinaangaliwa na rika zote kwani zipo familia ambazo hupenda kuangalia filamu wakiwa na watoto wao hivyo inakua jambo la fedheha pindi baba, mama na watoto kuona mambo yasiyo stahili kuangaliwa kwa pamoja kwani sisi ni waafrika ambao tunaheshimu jadi zetu ipasavyo.
Yaani ni hivi hata kama tukijidai eti tunawaiga wananchi waishio katika nchi za Magharibi huo utakuwa ni uzandiki mtupu tuige mambo yao lakini yawe mazuri naya maendeleo, kwani wao kuna mambo ambayo ni ya kawaida kwao lakini kwetu sisi ni mtihani mkubwa.
Kadhalika tukumbuke hata wao siyo kwamba wakati wote ni wakati wa kuonyesha tupu zao nao wana staha zao , jambo ambalo kwa kujidai tunaiga iga tutabaki kuwa malimbukeni wa fani tu hiyo wasanii mkubali mkatae itabaki kuwa hivyo.
Ushauri wangu mimi naona hakuna ulazima wa kuweka kipande hicho bora msiweke kabisa kwani kitaweza kuja kuua soko la kazi zenu ambazo tayari mmesha zipatia umaarufu ndani na nje ya nchi.
SERIKALI YATOA TAKRIBANI SHILINGI BIL. 41 KUBORESHA MIUNDOMBINU SUA
-
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Takribani shilingi bilioni 41 zimetolewa na serikali kupitia Mradi wa Elimu
ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaofadh...
4 hours ago
0 Comments