WAUGUZI WASABABISHA KIFO CHA MAMA MAPACHA UKONGA


Chalila Kibuda na Upendo Simon

Zahanati inayofahamika kwa jina la Community Oral Health (COH) iliyopo maeneo ya Ukonga Mazizini Jijini Dar es Salaam ambayo itoa huduma ya kuzalisha kina mama wajawazito wakati haina hadhi hiyo imesababisha kifo kwa mwanamke aliyekwenda kujifungua hospitalini hapo .
Tanzania Daima ilifika katika Zahanati hiyo na kujionea hali halisi ambavyo inaendesha huduma ya uzazi kwa wanawake wanaojifungua ambapo ilibainika haina uwezo huo na kusababisha kifo cha Mwanamke Issabella Mganga ambaye alifariki kutokana na kuishiwa damu baada ya kujifungua watoto mapacha kwa kile kilichodaiwa walimzuia kwenda kupata matibabu zaidi katika hospitali ya Amaana kwa sababu walikuwa wakimdai kiasi cha sh.158,000 za huduma waliyompatia.
Baada ya kujifungua watoto mapacha marehemu Issabella Mganga aliishiwa damu hali ambayo Zahanati hiyo ilishindwa kumpatia huduma ya kuongeza damu kwa mwanamke huyo, huku kifo chake kikiwa kimesababishwa na Zahanati hiyo kuthamini fedha zaiodi kuliko uhai wa mtu.
Akizungumza Tanzania Daima mmoja wa ndugu wa Maremu aliyejitambulisha kwa jina la Jairosi Mganga alisema kifo hicho kilitokana na huduma finyu inayotolewa hapo .
Alisema kuwa kutokana na masuala ya uzazi ambayo yanahitaji damu kulikuwa hakuna haja ya kupokea kama kulinda uhai wa mtoto na Mama.
Hata hivyo Mganga alisema kuwa Muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo alizidi kumchoma sindano tu bila ya kumuongezea damu mgonjwa huyo na alipoulizwa kwa nini hakumuongezea damu alisema pale wao hawana benki ya damu.
“Tunatoa huduma nyingi tu ikiwemo ya kuzalisha wakinamama lakini kuhusu kumuongezea mtu damu hatujihusishi na huduma hiyo”alisema muuguzi
Aidha ilidaiwa kuwa marehemu Isabela hawakupata ushirikiano wa kutosha wakati wa kujifungua .Baada ya kutokea tukio hilo Mmiliki wa Zahanati hiyo hiyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha na juhudi za Tanzania Daima kumpata zinaendelea.

Post a Comment

0 Comments