THE ACADEMY FOR KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS(2011)


Mtangazaji wa Redio 100.5 Time FM Dida ambaye wadau wamemzoea na kujipatia umaarufu katika miondoko ya Taarab kwa jinsi yeye anavyoipenda na kuufahamu vema muziki huo wa mwambao hasa Modern Taarab juzi usiku katika mnuso wa KTMA alitupiga mshangao kwamba yeye ni Mkali katika Kurap baada ya kugeuka kuwa MC Lyte kutokana na kuachia mistari ya wimbo wa 'Keep On' Wajina wewe ni Mkaliii.Swaga zake zimetufundisha wengi tusipende kusemasema kuwa unamjua mtu vilivyo kama ilivyokuwa kwa wana Academy kupigwa na mshangao kwa Kipaji alichokionesha Dida. Hapa akiendeleza kuchanqa mistari pia alicheza sawa na achezavyo MC Lyte. Hanifa Bonge mdau wa muziki akiwa na Mtangazaji wa Kipindi Cha Leo Tena kinachorushwa na Redio Clouds Gea Habib 'Mamaa wa Hekaheka'.
Watangazaji wa Luninga Maimatha Jesse TBC1 na Sauda Mwilima Star TV .
Mdau wa muziki, michezo na burudani Mboni Masimba na Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena kinachorushwa katika redio Clouds FM Dina Marios.
Adam Mchomvu DJ wa Redio Clouds, Frank Mtao na Mtayarishaji wa muziki Ally Baucha.
Kutoka kushoto ni Mtangazaji wa Redio One na ITV, Mdau Mboni Masimba na Mtangazaji wa Kipindi cha Emplifaya kinachorushwa katika Redio 88.4 Clouds FM Millad Ayo. Kushoto ni yule Jaji machachari wa Bongo Strar Search (BSS) ambaye amejizolea umaarufu na kupendwa na wengi Salama Jabir akiwa na mdau mwenzake katika KTMA .
Watangazaji kutoka luninga ya Channel TEN na Magic FM shoto Salma Msangi na Mishi Bomba 'Mishi B'.

Mimi na Grace .

Ben Kinyaia na Frank Mtao hawa nao walikuwa miongoni mwa wana Academy 100 ambao walikuwa na kazi kubwa ya kupitia kazi za wanamuziki.
Mwansasu na Bawazir.
Mrembo huyu nae ni Mtangazaji wa Redio Clouds hapa akiwakilisha Kampuni iliyoratibu mpango mzima ya One Plus.

Mimi na Kaka Abdallah Mwaipaya ambaye ni Mtangazaji wa Redio One na Televisheni ya ITV tulisoma wote shule moja tukakutana katika Academy.

Mtangazaji wa habari za burudani Sauda Mwilima akipozi kwa picha sehemu ya mapokezi hotelini hapo.
Fred Nyatori hapa akiwajibika katika kurekodi matukio yote yaliyojiri katika ukumbi huo.

Wakala Said Tuli 'Jirani A', Mwansasu 'Jirani B' na Bawazir 'Jiranii C' ndani wakia katika miongoni mwa wana Academy .

Beki wa zamani aliyepata kuchezea timu ya Yanga, Tanzania Stars Mwansasu, Wakala wa wachezaji wa Soka Said Tuli na Dativas Mango wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi.


Mdau Frank Mgoyo 'Dj Gonga' na Mtangazaji na mwanahabari Gerald Hando wakiwa wamejipunzisha katika varanda ya Kunduchi Beach.

Ulifika wakati wa kupata Chakula .
Mhariri wa Gazeti la Michezo na Burudani Grace Hoka na mimi hapa karibu vichwa vipasuke ka wazi ngumu tuliyokuwa nayo .Hii ni mara ya pili kuwepo na Academy ya KTMA ambapo mwaka jana ilifanyika katika katika kiota hichohicho na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).Pongezi kwao kwani katika tuzo za mwaka jana hakukuwa na malalamiko kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.Wana Academy100 walichangia katika kujadili kazi za wassanii zilizofanyika vizuri mwaka 2010.Majina ya wasanii watakaopigiwa kura kuwekwa hadharani siku yeyote kuanzia leo.kura zitaanza kupigwa Machi mosi na tuzo zitatolewa Machi 26 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Mchekeshaji Mpoki alikuweko katika Academy, lakini alilazimika kuondoka kwa kuwa nae alikuwa na wimbo unaogombea tuzo unaokwenda kwa jina la 'Shangazi'.
John Kitime akichangia katika moja ya hoja kwenye Academy
Brand Manager wa Kilimanjaro Beer George Kavishe na Mkurugenzi wa One Plus Communications, Fina Mango .
Msela wa akiwa viwanja vya Leaders alfajiri ambapo tulikuwa tukisubiri usafiri wa kwenda katika Academy Kunduchi.
Wajumbe wa Academy
Wajumbe wa KTMA kabla ya kwenda Kunduchi Bawaziri, Mimi niliemkaba ni Mtayarishaji wa Muziki Ally Baucha wa 'Baucha Records' Mussa 'Mtoto wa Uswazi'
Tayari kwa safari ya kuelekea Kunduchi Beach Hotel kwenye mkutano wa Academy wa siku mbili Jumamosi na Jumapili ndo tulikuwa huko kushoto kwangu ni mdau na mratibu maarufu wa matamasha ya bendi mbalimbali nchini Moody Bawaziri,mimi Omari Baraka na Mkala Fundikira.

Post a Comment

0 Comments