Social Icons

Friday, January 7, 2011

THT KUZINDUA ALBAM ZA WASANII WAKE NYOTA SITA MLIMANI CITY

KUHUSU MATALUMA
Mataluma anajulikana kwa ngoma yake maarufu sana “Kariakoo”,Mataluma ni moja kati ya wasanii wengi ambao wapo ndani ya nyumba ya vipaji (T.H.T),mataluma anajulikana kwa anina ya ngoma zake ambazo zinachezeka sana na kupendwa kusikilizwa na watu wengi.
Mataluma alizaliwa Mkoani Dodoma na kuanza sanaa kama mchezaji pale T.H.T Mataluma alipenda kucheza lakini mwisho wake alijikuta akipenda vyote; yaani kucheza na kuimba pia.
Mataluma mwenye staili ya pekee katika utunzi wa ngoma zake zinazochezeka na kugusa maisha ya watu ya kila siku na kuchanganya na midundo inayochezeka.
Kama hiyo haitoshi Mataluma anapenda muziki na kukaa kitaa, ndio maana mziki wake unagusa kitaa kwa njia mbalimbali na ni ambaye ameleta tena aina ya muziki ambao ulikuwa unapotea.
Ngoma yake ya Kariakoo ni kuhusu eneo la Kariakoo ambapo ni maarufu kwa wizi mdogomdogo wa mifukoni, ambapo wengi wetu tumeathirika nao kwa upande mmoja au mwingine.
JINA; Estellina Peter Sanga(Linah)
KABILA ;Mkinga kutoka Iringa
KUZALIWA; Machi 17, 1990
ALIPOZALIWA;Muhimbili hospitali,DSM.
ELIMU YAKE; Shule ya Msingi Ubungo Msewe 1998-2003 na 2004-2008 Shule ya Sekondari Msigani. 2009, mafunzo ya Kompyuta katika Kitengo Cha Kompyuta Cha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,(UCC).
ALBAMU YAKE; Albamu yake ya kwanza ilikuwa inakwenda kwa jina la ‘Ninakukimbilia’ iliyokuwa na vibao 10 vya dini.
MWASITI ALMASI
Jina: Mwasiti Almasi
Tarehe ya kuzaliwa: Februari 2, 1986
Alipozaliwa: Lugalo, Dar es salaam, Tanzania
Kimo: 5'7
Elimu: Mbezi Beach High School (alihitimu mwaka 2004)
Uraia: Mtanzania
Fani: mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na mwalimu wa uimbaji
Albam: Niambie (2008)
Mwasiti mwimbaji mwenye sauti kali, na mmoja wa wasanii wa kike wanaosisimua nchini Tanzania hivi sasa, ana miaka 4 tu katika tasnia ya muziki lakini amepata mafanikio makubwa kuzidi ndoto zake. Ameendelea kuwahamasisha wanamuziki waliopo na wanaojitokeza katika kuzifikia ndoto zao. Kwa mapenzi aliyonayo katika muziki, anawafunza vijana na wasanii wapya wanaojitokeza katika fani hiyo.
Katika mwaka wake wa kwanza katika fani, alitunukiwa kama msanii bora chipukizi na sasa ametoa wimbo bora wa mwaka katika mahadhi ya zuku (Nalivua Pendo) na Hao, wimbo wa kusisimua na uliopokelewa vizuri sana.
Mapema mwaka 2010 alisaini mkataba wa usambazaji na usimamizi wa utalii na kampuni ya SONY Afrika. Sony Afrika ni moja ya wasambazaji wakubwa kabisa wa muziki wa kiafrika duniani.
Akiwa mwenye mafanikio makubwa Mwasiti ameteuliwa kuwa balozi wa kupinga Malaria, akihamasisha kinga na tiba dhidi ya ugonjwa huo. Malaria haikubaliki ni kampeni
Kwa sasa ni balozi wa Maralia na amekuwa na ndoto za kusaidia maeneo yenye maambukizi ili kutoa misaada ya kuzuia.
Amekuwa akiimba matukio yanayoizunguka jamii kwa mfano wimbo wake wa ‘Niambie,’ ulimwezesha kutwaa tuzo ya malkia wa Zouk Tanzania na Afrika Mashariki kwa kupitia tuzo za Muziki za Tanzania mwaka 2008. na mwaka 22006 alitwaa tuzo ya mwimbaji bora wa kike anayechipukia.
Baada ya kumaliza shule ndipo alinza kujihusisha na masuala ya muziki, na hapo alijiunga na Nyumba ya vipaji Tanzania (THT).
KUHUSU FAMILIA YAKE
Baba na mama yake ni wenyeji wa Kigoma
MAFANIKIO
Mwanamuziki huyo amefanikiwa kushiriki katika Tamasha la Filamu la Zanzibar. Pia amewahi kushiriki katika tamasha la 10 la nchi za Ulaya.
WIMBO ULIOFANYA VEMA
Wimbo uliomtoa na kumtambulisha ni ‘Nalivua Pendo' ilifanikiwa kushika chati kwa kukaa kwenye chati kwa kukamata nafasi ya kwanza kwa muda wa wiki 30
KWA MUDA GANI AMEKUWA AKIIMBA?
Mwanadada huyo ameanza kuimba kwa muda mrefu kwani mama yake ndiye aliyevumbua kipaji chake mwaka 1995 wakati alipokuwa shule ya msingi.
WALIOMSHAWISHI KUIMBA
Wasanii waliomfanya ashawishike kuimba ni Lady Jaydee na Angelique Kidjo.
WATU MAARUFU ALIOWAHI KUIFANYANAO KAZI
Aliwahi kufanya kazi na waimbaji wa kimataifa kama: Latitudes wa Ufaransa, Bobby Ricketts wa Denmark, Angelique Kidjo wa Bennin, Zola wa Afrika Kusini, Lady Jaydee wa Tanzania na wengineo kibao wakiwamo wa nje.

Familia ya Linah ni ya kidini kutokana na ukweli kuwa baba mzazi wa Linah ni mchungaji wa kanisa .
Familia yake ina jumla ya watoto watano wakati Linah akiwa mtoto wa tatu kuzaliwa kutoka kwenye familia ya Mzee Sanga.
Familia anayotokea Linah ni familia iliyojaa wanafamilia waliojaa vipaji wenye vipaji vya kuimba.
MAISHA BINAFSI;
Linah ana anarafiki wa kiume ‘boyfriend’ ambaye ni mwana muziki mwenzake Amini, anaishi peke yake maeneo ya Kinondoni ambapo amepanga chumba.
Mbali na muziki pia Linah pia ni muigizaji kwani kwa sasa amesaini mkataba wa na clouds Tv ambako ataonekana katika tamthilia inayokwenda kwa jina la ‘69 Records’ ambayo itakuwa inarushwa na Clouds Tv.
MIPANGO YA BAADAE YA LINAH KIMUZIKI.
Mpango mkubwa na wa kwanza wa linah ni kurudi shule,na hii ni kutokana na ukweli kuwa yeye aliishia kidato cha nne tu,jambo lililochangiwa kwa kiasi kikubwa na matatizo yake ya kiafya.
Kama hiyo haitoshi pia Linah amepanga kukuza muziki wake na malengo yake ni kuufanya ujulikane Afrika nzima na Duniani kote.
MAISHA KABLA YA UIMBAJI
Kabla yakuanza uimbaji Lina alikuwa anajishughulisha na uimbaji wa nyimbo za injili lakini sehemu kubwa ya maisha yake ilikuwa ni shule kwa sababu ameanza muziki rasmi muda mfupi baada ya kumaliza shule.
KUHUSU DITTO
MAJINA KAMILI ; Doto Bernad
JINA LA KISANII ; Ditto
TAREHE YA KUZALIWA ; 8/1/1987
MAHALI ALIPOZALIWA ;Nshamba Bukoba lakini amelelewa Morogoro
UMRI ; 23
ELIMU ; Elimu ya msingi ameipatia Kiwanja cha ndege Morogoro kutoka 1993 mpaka 2000 kabla ya kujiunga na chuo cha ufundi kwa miaka miwili kutoka 2001 mpaka 2003.
UJUZI ; Mfua vyuma, kazi ambayo aliifanya kabla ya muziki akiwa anajihusisha na utengenezaji wa mabodi ya gari
ALBAM:Album yake ya kwanza inaitwa ‘WAPO’ ambayo ipo mbioni kutoka na itabeba nyimbo 10 mmoja wapo ukiwa ule utakaobeba jina la album, ‘Wapo’ na nyingine tisa.
nyimbo hizo ni ‘Kidogo’, ‘Kaluma’, ‘Ulisema’, ‘Kwa Pamoja’, ‘Nimechelewa’, ‘Sikumuelewa’, ‘Njaa ya Mapenzi’, ‘Alhamdullilah’ pamoja na ‘Mdomo’.
Nyimbo yake ya kwanza Ditto kurekodi ilikuwa ni ‘Darubini Kali’ akiwa na ‘Watu Pori’ chini ya Selemani Msindi ‘Afande Sele’.
Shoo yake ya kwanza kufanya ilikuwa ni katika onyesho la Sean Paul.
ALIKOTOKA
Ditto alikuwa mchezaji mpira, miongoni mwa timu alizo wahi kuchezea ni pamoja na Kingaru FC na Moro Kids zote za mkoani Morogoro. Vilivile Ditto ni mwamuzi wa soka.
Pia Ditto ameshawahi kufanya kazi moja kati ya viwanda vya kutengeneza bodi za magari kiwanda hicho kina julikana kama Inter mack kilichopo kihonda mkoani Morogoro.
KAZI ;
Kabla ya muziki alikuwa akifanya ufundi wa vyuma ambapo kazi yake kubwa ilikua ufuaji vyuma na kutengeneza bodi za magari,,,
-Kwa sasa ukiachana na muziki anafanya biashara Arusha ambapo ana maduka zaidi ya moja huko Arusha ambayo ni ya kuuza nguo za kike na kiume.
***********************************
Lile Tamasha kabambe la kufungua mwaka 2011 la kusherehekea miaka mitano ya Nyumba ya Kuvumbua vipaji nchini, Tanzania House Of Talent (THT), limekamilika.
Tamasha hilo litakaloambatana na uzinduzi wa albamu sita kabambe za wasanii mahiri wa miondoko ya Kizazi Kipya, limepangwa kurindima Januari 11, kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msemaji wa THT, Kemmy Mutahaba kiingilio katika Tamasha hilo bab’ kubwa, kimepangwa kuwa sh. 30,000, ambako ukumbi umeelezwa utameza mashabiki na wapenzi 400 tu siku hiyo. Tiketi zinauzwa katika Maduka ya Shearillusions yaliyopo Millenium Towers na Mlimani City pia tiketi zinapatikana katika Ofisi za Clouds FM Mikocheni na THT Kinondoni.
Albamu hizo sita zinazotarajiwa kuzinduliwa siku hiyo ni kutoka kwa wasanii wanaotamba vilivyo katika tasnia ya Bongo Fleva hivi sasa, Mwasiti, Amini, Dito, Barnaba, Lina pamoja na Mataluma. Licha ya kuzindua albamu zao, wasanii hao waliotokea kuwa gumzo hivi sasa wataudhihirishia umma kuwa wao ni wakali kwa kuonyesha laivu shoo ya aina yake jukwaani ili kuhakikisha wanakosha mioyo ya watakaohudhuria.
Mutahaba anasema kuwa, mambo mengi na kadha wa kadha, mapya na ya zamani kuhusu THT, ambayo wengi hawayafahamu yataanikwa siku hiyo kwa faida ya mashabiki na wapenzi.
Aidha, Mutahaba anasema kuwa, Tamasha hilo litapambwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa wasanii wengine mbalimbali nje ya kundi la THT.
Anawataja baadhi ya wasanii hao watakaopamba Tamasha hilo kuwa ni pamoja na Maunda Zorro, Banana Zorro, Pipi, Bendi ya Odama ma wanenguaji wa kundi la THT.
“Naamini kuwa, moto mkubwa wa burudani utawaka siku hiyo kwani maandalizi tuliyokwishayafanya ni makubwa,” anasema Mutahaba.
Zifuatazo ni dondoo fupi kuhusu wasanii wanaozindua albamu zao siku hiyo, ambao ni Mwasiti, Amini, Dito, Barnaba, Lina pamoja na Mataluma.
BARNA
JINA: Elias Barnabas
TAREHE YA KUZALIWA: 08/08/1990
MAHALI ALIPOZALIWA:Morogoro.
ELIMU YAKE;
1998-2004 elimu ya msingi Kinondoni shule ya msingi.
2005-2007 elimu ya sekondari aliishia kidato cha tatu.
ALBAMU YAKE;
Albamu yake ya kwanza aliifanya kwa kipindi cha kati ya 2008-2010 kwa ushirikiano na Amini iliyotambulika kwa jina la Njia Panda ambayo ilikuwa na jumla ya nyimbo 14 ambapo baadhi ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo ni pamoja na:
Njia panda: .iliyoimbwa naye Barnabas pamoja na Pipi
Muongo’ ,Robo saa, na Mbala mwezi zote zimeimbwa na Amini pamoja na Barnabas.
Wrong Number, iliyoimbwa na Barnabas pamoja na Linah
MAISHA YAKE KABLA YA MUZIKI
Baada ya kukatiza elimu yake ya sekondari alikuwa akitumia muda wake mwingi kuuza genge la vyakula lililokuwa nyumbani kwao pamoja na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki katika kanisa lao ambapo alipendelea sana kupiga Drums na gita.
KUHUSU FAMILIA YAKE
Familia anayotokea Barnaba ina jumla ya watoto watatu wakati Barnaba akiwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kutoka kwenye familia ya Mzee Barnabas.
MAISHA YAKE BINAFSI
Barnabas bado anaishi nyumbani kwao maeneo ya kigogo ambapo anaishi na familia yake.
Barnabas anamiliki duka linalouza vyakula lililopo maeneo ya Kinondoni .
Kila mwisho wa juma Barnabas huwa anapendelea kutembelea katika ufukwe wa bahari.
FALLY IPUPA ALIMSHAWISHI KUIMBA.
Barnabas alishawishiwa sana na msanii wa bolingo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) FallyIpupa , kuimba muziki kutokana na kuwa ni mwanamuziki pekee wa anayemvutia barani Afrika..
MBALI NA MUZIKI;
Mbali na muziki Barnabas anajihusisha pia na shughuli za biashara za uuzaji wa vyakula kwenye duka lake lililopo maeneo ya Kinondoni.
KWA MUDA GANI AMEKUWA AKIIMBA?
Barnabas amekuwa akiimba kwa muda wa miaka minne sasa tangu alipojiunga rasmi na T.H.T mwaka 2006 baada ya kupelekwa na rafiki wake wa karibu aliyekuwa anasali naye kanisani.
MIPANGO YA BAADAE YA BARNABAS KIMUZIKI
Mpango mkubwa na wa kwanza wa Barnabas ni kurudi shule,na hii ni kutokana na ukweli kuwa yeye hakuweza kubahatika kuendelea na masomo hadi ngazi ya juu ya kielimu.

JINA;Amini Mwinyimkuu
KABILA ;Muyao
TAREHE YA KUZALIWA;30/10/1986
MAHALI ALIPOZALIWA;Nyumbani,DSM.
ELIMU YAKE;
1997-2003 elimu ya msingiKinondoni shule ya msingi.
ALBAMU YAKE;
Albamu yake ya kwanza aliifanya kwa kipindi cha kati ya 2008-2010 kwa ushirikiano na Barnaba iliyotambulika kwa jina la NJIA PANDA ambayo ilikuwa na jumla ya nyimbo 14 ambapo baadhi ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo ni pamoja na ;
-Njia panda: iliyoimbwa naye Barnabas pamoja na Pipi
-Muongo: iliyoimbwa naye Amini kwa ushirikiano na Nyota Ndogo.
-Robo saa: imeimbwa na Amini.
-Mbala mwezi: Imeimbwa na Amini pamoja na Barnabas.
-Wrong Number: Imeimbwa na Barnabas pamoja na Linah
Kwa sasa Amini ndio anakamilisha albamu yake ya pili ambayo anabeba nyimbo zenye maadhi ya Zuku,rock na RnB,inayokwenda kwa jina la YAMETEKA DUNIA ambayo inabeba jumla ya nyimbo kumi ambazo ni ;
-Ndio unikimbie?: imetengenezwa naye Tuddy Thomas ndani ya Ngoma records.
-Mara ngapi?: imetengenezwa na Moses ndani ya Ngoma records.
-Subira: imetengenezwa naye Innocent ndani Ngoma records
-Yaniteka dunia(amemshirikisha Mwana FA): imetengenezwa na Innocent pamoja na Tuddy ndani ya Ngoma records
-Ungewaza: imetengenezwa na Matt Mzungu ndani ya Ngoma records
-Nilijua: imetengenezwa na Moses ndani ya Sound Crafter
-Sikumanya: imetengenezwa na Tuddy Innocent kutoka Ngoma records
-Ohae!!!(amemshirikisha Barnabas pamoja na Beka): imetengenezwa na Barnabas pamoja na Tudd
-Mama Emma: imetengenezwa na Tuddy pamoja na Barnabas ndani ya Ngoma records.
-Tumetoka mbali: imetengenezwa na Matt mzungu ndani ya Ngoma records

MAISHA YAKE KABLA YA MUZIKI
-Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi alikuwa akitumia muda wake mwingi kucheza mpira wa miguu na moja ya timu alizochezea ni NONDO FC iliyopo Kinondoni.
-Katika kujiongezea kipato Amini alikuwa akiokota mikaa iliyotupwa jalalani pamoja na vyuma chakavu.
KUHUSU FAMILIA YAKE;
-Familia anayotokea Amini ina watoto saba wakati Amini akiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa kutokea kwenye familia ya Mzee Mwinyimkuu.
Familia ya msanii Amini ni familia iliyojaaliwa vipaji katika kuimba
Kaka yake mkubwa ni Bahati (ambaye anapiga gita katika bendi ya Fablis band),
Bernadetha(anaimba kwaya kanisa la Roman Catholic), Kipara mfanyabiashara nchini Afrika Kusini, Julieth msusi, Dotto msusi,Maubii mfanyabiashara.
Amini: Baba yake Amini alifariki mnamo mwaka 1995 wakati Amini akiwa na umri wa miaka tisa na mama yake alifariki mwaka 2000 ambapo kipindi cha uhai wake alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga ngoma.
MAISHA YAKE BINAFSI
Amini hajaoa bali ana girl friend……Linah.
Amini anaishi peke yake maeneo ya kinondoni.
KWA MUDA GANI AMEKUWA AKIIMBA?
Amini amekuwa akiimba kwa muda wa miaka 11 sasa tangu aanze muziki ambapo wimbo wake wa kwanza kurekodi ulikuwa unaitwa Kino Mwaka 2006 ,Amini alibahatika kuchaguliwa kujiunga na T.H.T baada ya kupata ushawishi kutoka kwa msanii mwenzake anayefahamika kama Vumi.
MIPANGO YAKE YA BAADAYE YA AMINI KIMUZIKI.Mpango mkubwa na wa kwanza wa Amini ni kurudi shule,na hii ni kutokana na ukweli kuwa yeye hakuweza kubahatika kuendelea na masomo hadi ngazi ya juu ya kielimu

No comments:

 
 
Blogger Templates