SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI BINAFSI

Na Magreth Kinabo, MAELEZO
Serikali imeahidi kutoa ushirikiano na vyombo vya habari binafsi, huku ikivitaka vyombo vya habari nchini kuepuka kuandika habari ambazo zitakazoweza kuchochea vurugu .

Hayo yalisemwa leo katika mkutano wa mazungumzo kati ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi na wawakilishi wa Baraza la Habari (MCT) , wakiwemo Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari(MOAT), uliofanyika jijini Dares Salaam.
Mkutano huo ,pia ulimhusisha ,Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Funela Mkangara na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari ( MAELEZO), Rahael Hokororo.
“Hatuhitajia vikao rasmi mtoyeyote akiwa na jambo hasisite kufanya mawasiliano na Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo,. Mimi sitasita kukutana na nyie mara kwa mara”alisema Waziri Nchimbi.
Aidha Dk. Nchimbi alivitaka vyombo vya habari nchini kuandika habari ambazo hazitachangia kuleta vurugu huku akisisitiza kwamba vyombo vya habari vina umuhimu na mchango mkubwa katika kudumisha suala la amani na utulivu.
“Vyombo vya habari vikiamua nchi iwe tulivu itakuwa na Serikali itashirikiana navyo . utulivu tulionao haujatokea ulifanyiwa kazi ili uendelee kuwepo lazima ufanyiwe kazi,” alisisitiza huku akisema habari zinazoandikwa ziangaliwe ili kuepusha kuleta chuki katika jamii na kuangalia maslahi ya taifa.
Aliongeza kuwa Msemaji wa Serikali wa kila wizara, Watendaji wa Wakuu , Wakuu vya Vitengo na Maofisa wa Habari wake watakuwa huru kutoa habari mbalimbali ikiwa zitandikwa kama zilivyosemwa.
Alivitaka vyombo hivyo pia kujenga utamaduni wa watu kutoa maoni bila hofu bila ya kusababisha madhara katika nchi na kutenda haki kwa wanaozungumza nao.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa MCT, na Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi waliiomba Serikali kuhakikisha kwamba suala la Sheria ya Usimamizi wa Vyombo Vya Habari na Sera ya Habari vinafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.
Akijibu hoja hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ,Raphael Hokororo alisema sheria hiyo hivi sasa iko kwenye mchakato wa Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, wakati sera hiyo itarudi kwa wadau ili kuweza kupata maoni juu ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki katika sekta ya habari.
Naye Waziri Nchimbi alisema saula la sheria hiyo litafanyikwa kazi.

Post a Comment

0 Comments