Kiongozi wa bendi ya Jahazi Modern Tarab Mzee Yussuf amefanyiwa oparesheni ya mguu katika sehemu ya goti juzi katika ambapo amelazwa katika hospitali moja iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.Yussuf amesema kwamba kuumwa nisehemu ya uhai wa binaadamu hivyo amewatoa hofu mashabiki wake na kuwataka wajitokeze kwa wingi katika maonyesho ya Jahazi popote pale kwani ana hakika kwamba wasanii waliobaki watakonga nyoyo ipasavyo na hakutakuwa na pengo lolote."Ntashukuru endapo nitasikia mashabiki wangu wamefurika katika maonyesho ya Jahazi kama ninavyo kuwepo mimi kwani endapo watatjitokeza kwa wingi kiingilio chao ndicho kitakacho nisaidia katika kulipia matibabu" anasema. Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo Mzee (Mfalme) anasema alianza kusumbuliwa na goti mara baada ya kupata ajali wakati akiendesha Pikipiki akiwa Visiwani Zanibar.Kutokana na ugonjwa huo Mzee atalazimika kusugua benchi hadi hapo hali yake itakapo tengemaa na kuruhusu kurejea tena kazini.
WAMAJUMUIYA NEW YORK WAJUMUIKA KATIKA KISOMO NA DUA KUMWOMBEA MAREHEMU BABA
YAKE NY EBRA, BRONX, NEW YORK, NCHINI MAREKANI
-
*NY Ebra akifuatilia Dua na kisomo cha mpendwa baba Yake Mzee Abdallah
Nyagaly kilichofanyika siku ya Jumamosi tar ehe 21, Desemba, 2024 Bronx,
New York, ...
7 hours ago
0 Comments