DIAMOND NA G UNIT KUKAMUA CLUB MAISHA IJUMAA

Diamond akifurahia jambo na wasanii wenzake ambapo wote kwa pamoja kesho watakuwa Club Maisha.
Msanii Nassib Almas ‘Diamond’ , kundi la wasanii la P-Unit , Jo Makini na Code pamoja na Red Djs leo Ijumaa usiku wataachia burudani kamambe katika ukumbi wa Maisha Club uliopo Masaki Dar es Salaam ikiwa ni burudani ya kampeni ya kuwapigia kura za lala salama katika Tunzo za MTV Base Airtel MAMA’s.

Milango ya Club Maisha itafunguliwa kuanzia saa mbili kamili usiku na kiingilio kitakuwa sh. 20,000 kwa mtu mmoja.

Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari msanii Diamond amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi usiku wa leo ambapo amewaahidi kukonga nyoyo zao ipasavyo.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel ambao pia ni wadhamini , Kelvin Twissa alivitaja vyombo vya habari vitakavyokwenda kuripoti Tunzo hizo kuwa ni Redio One, Redio Clouds na kwa upande wa Magazeti ni gazeti linalotoka mara 2 kwa wiki la Championi na gazeti linalotoka kila siku la The Citizen.

Nao wasanii wa kundi la P-Unit ambao wanatamba na kibao cha ‘Maishani mwangu Sijamwoona Mkali’ wameomba Watanzania kuingia katika mtandao wa MTV ambapo watakutana na maelekezo ya jinsi gani ya kuwapigia kura.

Wakati huohuo wasanii wa kundi la G- Unit wamesisitiza na kusema kuwa ni jukumu la wadau wa ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuwapigia wasanii wanaowawakilisha kwani ushindi utakapopatikana siyo wa msanii au kundi wa waote.

Twissa alisema kuwa Diamond anawania Tunzo ya Msanii Chipukizi akiwa na wasanii wengien ambao ni Muthoni (Kenya), Jojo (Gabon) na Mo Cheddah (Nigeria). Diamond anatarajiwa kuondoka nchini Desemba 8 kwenda Lagos Nigeria ambapo hafya hiyo itafanyika Desemba 11 mwaka huu.
Shostito Mamaa Cecy Jeremiah na mimi katika mkutano huo tukipoza makoo baada ya mkutano
Cecy na Diamond hapa wakipozi kwa picha.
Baada ya mkutano ukafika wakati wa tukio muhimu maishani hapa nikawa najipendelea kwa chakula ninachokipenda maishani mwangu ni ugali kuku, matembele ,njegere na kachumbari.

Post a Comment

0 Comments