Naibu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Jacky Mugendi Zoka akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar wakati alipotoa taarifa ya kupinga madai ya Dk Willbrod Slaa Mgombea urais wa CHADEMA kuwa idara hiyo imeshiriki katika kuchakachua Kura za mgombea huyo wa urais. Naibu Mkurugenzi huyo amesema wananchi wampuuze Dk Slaa kwa kauli yake kwani madai yake hayana ukweli wowote na ameongeza kwamba idara yake haijajihusisha kabisa na masuala ya uchaguzi hivyo madai hayo ni ya kuipaka matope idara hiyo.
SERIKALI YATOA MILIONI 400 KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI KWA RUZUKU DODOMA
-
Mitungi 19,530 kuuzwa kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuhamasisha na
kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia
Chamwino - Dodoma
WAKALA wa Nishat...
1 hour ago
0 Comments