MAMIA WAMZIKA SILLERSAID MZIRAY

Mjane wa Marehemu akiwa na ndugu wa marehemu katika ibada kabla ya maziko iluyofanyika kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni na baada ya hapo mwili wa SillerSaid Mziray umepumzishwa katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam leo jioni ambapo mamia ya wakaazi, watu wa kada mbalimbali wanamichezo wamehudhuria maziko hayo
Kina mama nao walikuwa wengi sana hapa wakiwa katika foleni ya kuuaga mwili wa Marehemu.
Viongozi wa Michezo nchini kutoka kushoto Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodgar Tenga, akifuatiwa na Kamishna Mkuu Mstaafu pia Luteni Kanali Mstaafu Idd Kipingu,Mjumbe wa Heshima Wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Said El Maamry na Naibu Mkurugeni wa Michezo nchini Juliana Matagi Yasoda.
Marehemu SillerSaid Kahema Kagela Mziray ameacha mke na watoto 2 huyu ni mmoja wapo mwingine ni wa kike anaitwa Miriam.
Mjane wa Marehemu SullerSaid Kahema Kagela Mziray.
Ndugu na jamaa wakilia kwa uchungu wakati wa kuuaga mwili wa marehemu
Padre akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Kocha wao.
Meneja wa Klabu ya Yanga 'Young African' Emmanuel Mpangala.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Kaburu Nyange.
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni.
Mjumbe wa Heshima wa CAF Said Elmaamry.
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania Mohammed Mpinga.
Le Maestro , Kassim Mapili akiaga mwili wa marehemu Mziray kwa uchungu.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga alitoa pole kwa wafiwa wote huku akisema kwamba kifo cha Mziray ni pigo kwa wanasoka Tanzania kwa ujumla na kumsifu marehemu alikuwa mtu mwenye msimamo na kujenga hoja katika jambo aliloliamini, mchambuzi wa soka aliyelipa Taifa heshima. Huku akibainisha kwamba wanasoka wote nchini watamkumbuka daima.
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Lyoid Nchunga katikati akizungumza na wadau.
Hakika siku misiba hukutanisha watu kushoto ni Suleiman Matola na Asha Muhaji a.k.a Sister Asha wakifurahi pamoja baada ya kupotezana kwa muda mrefu.
Suleiman Matola hapa mara baada ya kuuaga mwili wa Super Coach.
Kutoka kushoto ni Kalili, Matola na Muhaji.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Hassan Dalali naye alikuwepo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga L.Nchunga hapa akizungumza na kutoa sifa za aliyekuwa Super Coach ambapo alibainisha kwamba hata wao Yanga wamepata pigi kubwa huku wakitangaza kutoa ubani wa kiasi cha sh. 500,000 kwa familia ya marehemu.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Davis Mosha akiteta jambo na wadau.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Kaburu Nyange akitoa wasifu wa marehemu SillerSaid Mziray.
Mwili wa Marehemu ukiwasili katiwa viwanja vya Biafra mchana wa leo.
Mtoto wa Marehemu na Kaka wa marehemu wakifuatilia misa.
Kaka wa marehemu Salum Mziray.
Hapa ni kiwanja cha Biafra Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo ndipo paliendeshwa ibada ya mwisho ya safari ya SillerSaid Mziray.

Post a Comment

1 Comments

Anonymous said…
Kweli tunakushukuru kwa taarifa na taswira hizi. wito wangu kwako ni kwamba uwe makini na majina ya wahusika katika picha. kwa faida yako anayeuaga mwili wa hayati mziray kwa kuubusu ni Mzee Kassim Mapili mwanamuziki mkongwe hapa nchini na wala sii maestro King Kikki kama ulivyoeleza. RIP MWANANGU!