Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC Jaji Lewis Makame kushoto na Mkurugenzi wa Tume hiyo Rajab Kiravu wakijadiliana jambo mara baada ya kutangazakura za uaris katika majimbo mengine 24 leo asubuhi kwenye kituo cha kutangazia matokeo hayo. Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ulifanyika jumapili iliyopita nchini kote ukishirikisha vyama mbalimbali vya siasa, Mpaka sasa tume ya uchaguzi tayari imeshatangaza matokeo ya urais katika majimbo 201 yakiwa yamesalia majimbo 38 ili kukamilisha kazi hiyo. Mkurugezi wa Tume ya Uchaguzi Rajab Kiravu amesema huenda tume hiyo imamalizia kutangaza majimbo hayo 38 yaliyosalia jioni ya leo kuanzia saa kumi jioni wakati watakapotangaza majimbo yaliyobaki, lakini pia amesema watajibu maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari baada ya kumaliza kazi hiyo.
MWENYEKITI COREFA AJIFUNGA MKANDA KUFUFUA SOKA LA UFUKWENI PWANI
-
NA VICTOR MASANGU,PWANI
Chama cha soko Mkoa wa Pwani (COREFA) katika kuunga mkono juhudi za Rais wa
awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza se...
12 hours ago
0 Comments