Na Samia Musa
Serikali leo imewasihi wanawake watakaoshiriki katika mashindano ya dunia ya Gofu ya wanawake kufanya jitihada na kurejea na ushindi katika mashindano ya dunia yatakayofanyika Argentina kuanzia Oktoba 20-23.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya gofu jana, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo alisema wasikatishwe tamaa na lolote na badala yake kuongeza morali na kurejea na ushindi wa mashindano hayo.
Thadeo alisema ushiriki wa wanawake katika mashindano hayo ni historia kwa sababu ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki kutokana na juhudi za rais wa mchezo huo Jamal Malinzi aliyefanikisha ushiriki huo. “Ushiriki wetu katika mashindano hayo ni historia kwa Tanzania, nafahamu juhudi za kukuza mchezo huo zimeanza siku nyingi na hadi kupata nafasi ya ushiriki ni mwanzo mzuri wa maendeleo,”Naye Rais wa Gofu wanawake, Mbonile Burton ikiwa ni mara ya kwanza Tanzania kushiriki anashukuru kupata hiyo nafasi ambayo ni adimu, watatumia nafasi hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo. Burton aliwataja wachezaji hao ni pamoja na Hawa Wanyenche ambaye ni nahodha wa mchezo huo na Madina Idd ambao wataongozwa na Burton ambako wanaondoka kesho kuelekea nchini humo.Naye Wanyenche alisema watatumia fursa hiyo kurejea na ushindi wa mashindano hayo wakiwaahidi Watanzania watafanya vizuri katika mashindano hayo na kuwashukuru waliofanikisha safari yao.
JENGO LA MAKAO MAKUU WMA KUKABIDHIWA FEBRUARI 10, 2025, UJENZI WAFIKIA
ASILIMIA 95.2
-
Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil
Abdallah,ameridhishwa na ujenzi wa Jengo la Wakala wa Vipim...
35 minutes ago
0 Comments