Social Icons

Thursday, May 5, 2016

MSANII SNURA MUSHI AJITOKEZA KUOMBA MSAMAHA MBELE YA WATANZANIA KWA VIDEO YAKE YA 'CHURA' KUKIUKA MAADILI YA KITANZANIA

 Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK (kushoto) akisoma taarifa ya Snura Mushi kuomba msamaha kwa Watanzaniaya kutokana na kusambazwa kwa video ya msanii huyo iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
      PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi (kulia) akiomba msamaha mbele ya Watanzania kutokana na kusambaza video yake iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK

NA KHADIJA KALILI

Ikiwa  ni siku moja tu tangu Wizara ya Habari , Utamaduni Sanaa na Michezo  jana kutangaza  kumfungia msanii  Snura Mushi  kujihusisha na masuala ya sanaa  ikiwemo kutumbuiza kutokana nawimbo wake wa Chura ambao aliusambaza kwenye mitandao ya kijamii You tube, WhatsApp na mingine mingi kutokana na kurekodiwa kinyume na maadili ya Mtanzania.

Ndipo leo asubuhi Snura alipoibukia kwenye Ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari MAELEZO,Jijini  Dar es Salaam na kuzungumza na vyombo mbalimbali vya habari.

Baada ya kuwasili ukumbini na kutambulishwa Snura alianza kwa kusema "Karibuni  ndugu zangu  waandishi wa habari , naitwa Snura Anthony Mushi  wengi  wananifahamu  kwa jina la  kisanii  Snura,  na kulia kwangu  ni msimamizi  wa kazi zangu  za sanaa 'Meneja' wangu Hemed Kavu almaarufu  kwa jina la HK.

Kwanza  tunatanguliza shukrani  zetu za dhati  kwa kuitikia wito huu:
"Tumewaita hapa leo kwa ajili  ya kuomba  radhi  umma wawatanzania  kwa ujumla  kwa kosa l;a  kutengeneza , kuzindua  na kuweka  mtandaoni video ya udhalilishaji  wa  mwanamke  isiyozingatia  maadili  ya kitanzania ya muziki unaoitwa 'Chura' alisema Snura.

"Tunaviomba radhi  vyombo vya serikali  vinavyosimamia  sekta  ya sanaa kwa  kutofuata  sheria , kanuni na taratibu zilizopo  katika  uendeshaji wa sanaa nchini".

"Mimi na Meneja wangu  tunaahidi  kutorudia  tena kufanya  tukio  hilo la udhalilishaji , na iwapo  tutarudia  basi tupewe adhabu  kali kwa mujibu wa sheria za nchi hii" alisema Snura.

 Aliendelea kwa kusema kuwa  "pia tunaahidi  kuwa mfano bora  kwa jamii  inayowazunguka   na kwa wasanii  hususan katika masuala yahusuyo  kutunza na kufuata  maadili  na utamaduni  wetu pamoja na  sheria za nchi. Hii ni pamoja na  kupata vibali  katika  mamlaka na taasisi zinazohusika".

Katika hali isiyokuwa ya kawaida pia Snura amekiri kuwa alikua akifanya shughuli zake  za sanaa bila ya kuwa  na usajili  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

"Tunafahamu kwamba baadhi ya wasanii hususan wa  muziki wa kizazi kipya  hawajajisajili   BASATA  kama ilivyokuwa kwangu mimi  lakini kwa sasa  baada ya  kupata maelekezo  kutoka (BASATA), nimeshapata usajili  na sasa natambulika kisheria.
    
Snura aliweka wazi kuwa yeye binafsi aliitwa  Wizarani na kuhojiwa kuhusu wimbo wake wa Chura hivyo  alitambua kwamba utafungiwa akagundulika hakuwa na usajili  BASATA.

Alisema sharti la kwanza alilopewa ilikuwa ni kuitoa video  ya Chura kwenye mitandao ya kijamii  You Tube  kutokana na namna ilivyorekodiwa." Tayari  hili limeshatekelezwa  na video imeshafutwa kwenye akaunti hiyo. alisema HK.

Pia tayari Snura ameshasajiliwa BASATA  hivyo yuko huru kufanya kazi  katika maonyesho  yake ya sanaa .

Akizungumzia kuhusu sharti la tatu  ni  kuiirekodi upya  video  na muziki ya Chura.

KWANINI CHURA  IMEMDHALILISHA SNURA?

Kwa mujibu wa Snura anakiri ni kutokana na kiwango kidogo cha elimu alicho nacho pia upeo wake wa kufikiria ndiyo ulifikia ukomo hivyo asamehewe.

"Mimi sikuwa na lengo la kuwadhalilisha  wanawake wenzangu kukatika viuno hapa kwetu ni jadi na mimi mwenyewe nacheza , kuhusu nguo kulowekwa maji  alisema kuwa wale walivaa mitandio na walilowa maji huku akisisitiza kuwa waliona mazingira ya maisha ya Chura ni kwenye maji hivyo wao waliona sawa kujitumbukiza kwenye maji.
 
"Lakini jiliporudi nyumbani  na kuiangalia vizuri video ya Chura nikaona ina makosa ndiyo maana sikuisambaza kwenye Luninga yoyote" alisema Snura.

Mwisho msanii huyo  pamoja na Meneja wake  wametoa shukrani  za dhati  kwa Wizara  ya Habari , Utamaduni , Snaa na Michezo  pamoja na BASATA kwa ku maelekezo  na elimu  waliyowapatia.

Juku wakiahidi  kufanya kazi  na kuwa mabalozi  wema kama walivyoagizwa.

   "Hivi sasa tunaufanyia masahihisho wimbo wa Chura  pamoja na video yake na baada ya hapo utaangaliwa na Bodi ya Filamu

No comments:

 
 
Blogger Templates