Social Icons

Thursday, February 10, 2011

TWANGA WATOA RAHA CLUB BILICANAS USIKU WA KUAMKIA LEO

Asha Said 'Sharapova ' mnenguaji machachari na anayevutia jukwaani akiwa kazini.
Maua ya Twanga hapa yakionyesha mtindo wa kutwanga .
Huyu ndiye anayepagawisha manake muziki bila ngoma hauwezi kuoga anaitwa MC D hapa akiwajibika jukwaani.
Wapalestina nao wamooooooo.
Baada ya kutandikwa golo moja na Timu ya Taifa Stars wachezaji wa timu ya Palestina walijifuta machozi kwa kuwemo katika Club Bilicanas ambapo walikaribishwa jukwaani wakasugua kisigino katika mtindo wanaoujua wao sijui walikuwa wakielewa kilichokuwa kikiimbwa au la lakini la muhimu ni kwamba waliweza kufuata midundo. Mbali ya Wapalestina kuwa kivutio kwa muda mfupi jukwaani , Pia uongozi wa ASET ulimtangaza Greyson Semsekwa na Khadija Mnoga Kimobitel waliojiunga na bendi hiyo.
Muimbaji kiraka na mwenye mvuto Charlz Baba akifuatiwa na Kiongozi wa bendi mwanamama Luiza Mbutu'Mama B' hapa wakiimba katika onyesho la o linalofanyika kila Jumatano katika Club Bilicanas.Onyesho hilo linalopendwa na wengi licha ya kuwa katikati ya Juma lilifurika wati wengi Mashuhuri nchini, wasanii wa filamu wasanii kutoka bendi mbalimbali na wafanyabiashara maarufu Jijini Dar es Salaam ambapo kila mmoja alikuwa akipagawa kivyake.
God Kanuti mpiga gitaa.

Ray Kigosi na Aunt Ezekiel nao walikuwepo.

No comments:

 
 
Blogger Templates