KATIBU MKUU CCM DKT. ASHA ROSE- MIGIRO AFUNGA MKUTANO WA 12 WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika wamepitia maazimio ya mkutano wa 12  Wakuu wa nchi za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika uliofanyika nchini Afrika ya kusini mwaka Jana ambapo wamekubaliana kuangalia mabadiliko ya jiopolitiki ,siasa, uchumi na maendeleo katika nchi za Afrika zilipo Kusini mwa Afrika.

Hayo yamesemwa Jana na KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Dkt.Asha Rose Migiro ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mkutano huo wa siku mvili uliofanyika katika Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Julius Kibaha Mkoani Pwani ambapo Makatibu Wakuu wa nchi sita zilizoshiriki harakati za kupigania Uhuru za Kusini mwa Afrika.

Dkt. Migiro amesema maazimio hayo yalihusu kuangalia hali ya kisiasa katika eneo la kusini mwa Afrika na kuangalia ni namna gani wanakwenda nje ya lengo la kwanza la ukombozi ambalo lilikuwa ni kupata Uhuru wa bendera ambapo jukumu lao kubwa kwa sasa ni kuhakikisha tunachochea maendeleo ya kiuchumi na jamii.

 "Vile vile katika  mkutano wa 11 uliopita waliazimia nchi zetu ziimarishe uhuru wake sio tu uhuru wa bendera na uhuru wa uchumi Bali ni uhuru wa kwa pamoja kama nchi za kihistoria zilikuwa pamoja na kuangalia changamoto zilizopo sasa hivi.

"Kuna mabadiliko ya kiniopolitiki, migogoro huku na kule na kuangalia nchi zetu zinasimama imara vipi kwa kukabiliana na migogoro mbali mbali inayotokana katika nchi zingine.

"Hilo ni.eneo kubwa ambalo tumezungumza yaani masuala ya siasa, uchumi na maendeleo ya kijamii katika eneo letu la ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika ili kuhakikisha uhuru tuliopata unaendelea kulindwa na unahimalishwa na juhudi za kuwatumikia wananchi" amesema  Dkt. Migiro. 

"Katika Hilo nchi zetu zimefanya mapitio ya maendeleo mbali mbali yaliyotokea katika nchi zetu kwa mfano kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumezungumzia jitihada za kuendeleza miundombinu na kuhimarisha huduma za jamii na kuweka mikakati ya kujenga uchumi stamilivu ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

"Kwamba hayo tunahakikisha yanakwenda sambamba na uhuru tuliopata na sasa ni wakati wa kuhimarisha umadhubuti wa jitihada zetu tulizofanya tangu tuliopata uhuru kwa upande wetu CCM na nchi zingine" amesema Dkt. Migiro.

Aidha kwa upande wa wenzetu wametueleza kuwa vyama vingi vinazungumzia changamoto ya ajira kwa vijana, haja ya kuweka mikakati ya kuangalia changamoto ambazo zinawahusu sana vijaya na wanakuwa sehemu kubwa ya jamii ambalo limeonekana katika nchi zetu zote hizo ambazo tumezungumzia kupitia majukumu ya kisiasa.

"Hivyo wanajioanga kuitafutia utatuzi pamoja na mabadiliko ya tabianchi huku wakitolea mfano hai kwa nchi ya Msumbiji ambayo imekua ikikumbwa na gharika za mvua kubwa na vimbunga mara kwa mara ambapo kwanza wameshukuru wakati wa matatizo yao tulikuwa pamoja nao lakini pili tuendelee kuwekeza katika zile shughuli zinazozingalia mabadiliko ya tabia nchi" 

"Wenzetu wa Afrika ya kusini, Namibia, Zimbabwe hawakuwa na kitu tofauti na tulivyotoa kwamba nchi zetu zinakabiliwa na ongezeko la vijana, changamoto za upatikanaji wa ajira, haja ya kuwawezesha wanawake kwani imeonekana kwamba wanawake ni sehemu nzuri ya uchumi wa nchi zetu na ni sehemu muhimu ya ukombozi wa bara la Africa kwa hiyo tuendelee kuhimarisha mikakati ya kujenga jamii jumuishi, uchumi jumuishi na uchumi stamilivu.

Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS),kikao kilichoketi tarehe 4 na 5 Machi 2026, Kibaha, Mkoani Pwani. 

Wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho ni; Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU-PF (Zimbabwe), Jacob Francis Nzwindamilimo Mudenda, Chama cha SWAPO (Namibia), kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dkt. Samuel Abraham Peyavali Mushelenga na Chama cha MPLA (Angola) kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederico Toth Jorge De Miranda.

Post a Comment

0 Comments