Na Khadija Kalili, Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kuacha tabia ya urasimu wa kufanya maamuzi yenye tija kwani yamekua Haya wawekezaji pia ni kero kwa wananchi.
RC Kunenge amesema hayo alipozungumza na viongozi hao katika kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa ahadi za kuelekea siku 100 za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan .
Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Desemba 2025 kwenye Ukumbi wa Mikutano Mkoani hapa.
"Kila kiongozi ana wajibu wa kuhakikisha kwamba urasimu unaondoka ndani ya Mkoa wetu ili tuweze kuleta maendeleo naagiza nendeni mkasimamie ndinyi ndiyo
Watendaji acheni urasimu wa kukwamisha mambo mbalimbali ndani ya Mkoa ".
"Bajeti ya nchi ni 1.9 ni misaada na inakwenda kupungua kutokana na changamoto tuliyoipitia hivyo tujipange kuziba pengo hili aidha kwa kuongeza kukopa ama kuzalisha , tufanye kazi kitaalam tusipoteze muda na rasilimali za Mkoa asilimia 20% ya utendaji wetu unapimwa na asilimia 80% ya matokeo yetu,kafanyeni maamuzi kwa wakati" amesema Kunenge.
Akizungumza kuhusu kujipanga uwasilishaji wa utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Mhe. Rais Samia kwamba wameangalia katika maeneo ya Mkoa na namna watakavyotekeleza ili utakapofika wakati wa kuwasilisha wakawasilishe vyema katika ngazi ya maeneo yanayohusu Mkoa wa Pwani na kusisitiza kutoa taarifa zilizo sahihi.
"Tunafahamu kuwa Rais Dkt. Samia atatekeleza ahadi zake alizozitoa ndani ya siku 100,jambo kubwa ni kuhakikisha na sisi tunatekeleza ya kwetu katika ngazi ya Mkoa, japo kuna mambo ya kisera,kitaifa ,
Mkoa, Wilaya na Halmashauri bila kujipanga na kujua yapi ya kufanya tathmini kutekeleza mikakati ili muda utakapofika tuwasilishe kwa weledi wa hali ya juu"
Wakati huohuo Baraka Mwambange ambaye ni Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Pwani (TANROAD) amepewa tuzo ya kutambua mchango wake katika utendaji wa kazi zake amabapi amehakikisha na kusimamia barabara za Mkoa wa Pwani zinapitika katika kipindi chote.
"Barabara na madaraja sawa na mishipa ya damu kwa binadamu ,hii ni mara ya kwanza kutoa tuzo na itamjengea ari ya kuchapa kazi zaidi muhusika" amesema Kunenge.
"Tutaendelea na utaratibu wa kutambua kazi za watumishi wa umma ambao wataonekana kufanya kazi zao kwa weledi na tunatakiwa kutambua kila mtumishiin anapofanya jambo jema huwa tunawaandikia barua na kupelekwa wakuu wake wa Idara pia barua hiyo huwekwa kwenye faili lake ikiwa linaambatana na taarifa zake za kumbukumbu katika kazi" amesema RC Kunenge.
RC Kunenge amesema kuwa mbali ya tuzo hiyo pia wamemuandikia barua ya pongezi na nakala imekwenda kwa viongozi wake.



0 Comments