Na Mwandishi Wetu Zanzibar
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimebainisha kuwa hakuna uchaguzi utakaorudiwa wala serikali ya mpito itakayoundwa kama inavyodaiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwani taratibu zote zilifuatwa.
Kupitia Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche chama hicho ambacho kilisusia uchaguzi mkuu uliopita hivi sasa kinadai kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii, kuundwa serikali ya mpito, kuvunjwa Tume Huru ya Taifa Uchaguzi na kurudiwa uchaguzi mkuu uliopita 29 Oktoba 2025.
Akizungumza mjini Unguja 16, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar. Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema serikali ya mpito huundwa pale kunapokuwa na tatizo mathalani Serikali au Tume ya Uchaguzi imekiondoa chama kwa mizengwe au madai ya kutoshindwa kihalali.
Alisema mwenezi huyo kuwa kabla ya kufikia uchaguzi kuna hatua chama kinatakiwa kufuata na uchaguzi umefanyika, vyama 18 vimeshiriki na chama kimoja hakikushiriki na ndio kinataka kunishurutisha vyote jambo ambalo haliwezekani.
Alisema Mbeto kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na inafuata katiba ambayo inasema uchaguzi utafanyika kila baada ya miaka mitano.
"Wakati ulipofika wao wenyewe walikataa kushiriki kupitia tamko la Kamati kuu ya chama hicho na wakaja na kauli, No reform No election kisha wakadai watakinukisha" alisema Mwenezi Mbeto.
Chadema hakikushiriki kwa msimamo wa chama chao, tena wakatoka wazi na kudai hadi ipatikane tume huru ya uchaguzi ambayo ndio hii iliyopo, inatekeleza majukumu yake na ina ukomo wake" alisema.
Ukomo tume hiyo kikatiba itahudumu hadi pale itakapo 2027" alisema.
"Chadema wana sababu gani za kutokushiriki?kulikuwa na vita?" alihoji Mbeto.
Alieleza kuwa sheria ya msajili wa vyama inasema vyama vyote vina nafasi sawa na kama 18 vimeshiriki vipi kimoja ndio uchaguzi urudiwe, jambo hilo alisema haiwezekani.
Alisema sheria zimefuatwa kwa mujibu wa katiba na asilimia 97 ya waliopiga kura wamemchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, hakuna mjadala kwani serikali tayari imepatikana na uchaguzi ujao 2030" alisema Mbeto.
Alibainisha kuwa chini ya R za maridhiano za Rais Samia, CCM ipo tayari kama kuna jambo la kiTaifa kuzungumza, kusikiliza na kujadili mapungufu ili kuona jinsi ya kupeleka mbele Taifa lakini sio serikali ya mpito wala kurudia uchaguzi kwani umemalizika hadi mwingine 2030.

0 Comments