Na Mwandishi Wetu, Mafia
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeongeza mitambo miwili ya uzalishaji umeme katika kituo kikuu cha umeme wilayani Mafia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kupitia TANESCO za kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote. Mitambo hiyo ina uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati mbili ambapo kila mtambo mmoja utazalisha megawati moja. Akizungumzia juu ya mitambo hiyo, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mafia Mha. Seif Kijanga amesema, “Katika Wilaya yetu ya Mafia hivi karibuni tumepokea mashine mbili, mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme megawati mbili tunatarajia baada kukamilika ufungaji wa mitambo hii tutakua na upatikanaji mzuri wa umeme wa uhakika”. Kwa upande wake Mhandisi Mariam Patrick, ambaye ni mratibu wa mradi alieleza kuwa ujio wa mitambo hiyo ni ushahidi wa dhamira ya Shirika katika kuboresha huduma kwa wananchi. “Kupitia mitambo hii, tumeongeza uwezo wa uzalishaji mara mbili zaidi ya awali.



0 Comments