Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaja mgombea wake wa Urais Zanzibar Rais Dkt. Huseein Ali Mwinyi miaka mitano iliopita amekuwa dira na ramani iliofikisha Zanzibar katika uwanja mpana wa maendeleo.
Pia chama hicho, kimesifu juhudi na utendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na jina la Dkt. Mwinyi limeingia katika rekodi ya utumishi uliotukuka.
Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi,mUenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema Zanzibar ya Mwaka 2025 kimaendeleo si ya mwaka 2020.
Mbeto alisifu utendaji wa pamoja wa SMZ na kuitaja miradi mikubwa ya kisekta ilioanzishwa na kukamilika, hivyo maendeleo yaliopatikana yatabaki kuwa alama isiofutika.
Alisema kutokana na utendaji wa serikali ya awamu ya nane ya Rais Dkt. Mwinyi amefuata nyayo na urithi na matunda ya watangulizi wake katika kusimamia maendeleo ya nchi na watu.
" Rais Dkt. Mwinyi atabaki kuwa mfano na kielelezo cha utumishi bora. Miaka mitano ya serikali yake ametimiza wajibu kwa wananchi na kufanya mageuzi makubwa katika ustawi wa jamii" alisema Mbeto.
Katibu huyo Mwenezi alisema licha ya uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi kuwa kama dira na ramani iliofikisha mbali Zanzibar kimaendeleo lakini pia wananchi waishi kwa upendo na umoja.
"Serikali ya awamu ya nane Zanzibar imekomesha maonevu, ubaguzi na upendeleo. Rais Dk Mwinyi amekataa kuongoza kwa visasi na chuki Serikali yake imewajibika na kutumikia wananchi" asisitiza.
Pia Mbeto alisema hakuna jambo lolote litakalomzuia asirudi tena ikulu, kwani alioyaahidi ameyatekeleza ikiwemo kuondosha changamoto alizozikuta na kufanikisha miradi ya kisekta.
"Wananchi ili kumtuza Rais Dk Mwinyi wameahidi kumpigia kura nyingi ili akamilishe kazi alioianza mwaka 2020. Mgombea Urais wa CCM hana deni kwa wananchi wake" alisema Mbeto.

0 Comments