Na Mwandishi Wetu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Hassan Serera amewaasa wahitimu wa mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Taasisi za Umma (SLM-PESA) pamoja na Vijana kwenda kupigatia Afya ya Akili katika ofisi wanazo fanyakazi na wanaowaongoza kwa ujumla.
"Ukiwa Kiongozi mnao wajibu wa kwenda kuzingatia elimu mliyopatiwa ilikukabiliana na changamoto hii ambayo inaonekana kuwepona kuitafutia utatuzi kwa hekima" amesisitiza Dkt. Serera.
Dkt.Serera amesema hayo alipokua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo hayoya siku sita yaliyofanyika tarehe 29 Septemba na kuhitimishwa Oktoba 4 Mwaka huu katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani .
Amesema kuwa mafunzo haya yakawe chachu ya kugundua wenye shida ya Afya ya Akili na kutatua kwa hekima ya hali ya juu huku lengo likiwa kujenga na siyo kubomoa huku akisisitiza kwa kusema kuwa ,kuwaandikia barua kali na zenye kutoa maonyo siyo suluhisho sahihi,tafuteni njia mbadala hasa katika kuzungumza zaidi" amesema Dkt.Serera.
"Tafuteni njia mbadala ya kukabiliana na wafanyakazi ambao wanapitia changamoto ya Afya ya Akili lugha za ukali huzidisha tatizo" amesema Dkt. Serera.
Amesema kuwa wahitimu hao waende kuitendea haki elimu ambayo wamepatiwa ya namna ya kukabiliana na changamoto hiyo.
"Tulivyoingia ni tofauti na tunavyotoka kwa sababu tunashukuru tumejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na Uongozi wa kimkakati ulinzi wa nchi ambapo ni pamoja na kulinda mali za nchi ambao ndiyo chakula cha nchi, kuwa wazalendo ni jambo la msingi, Itifaki na mengineyo mengi .
"Tunaahidi kujenge utamaduni wa kwenda kueleza yale yote ambayo tumefundishwa hapa" amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Profesa Marcellina Mvula Chijoriga, John Baitani amesema walipokea maombo 300 lakini ni 29 waliyomudu kujilipialicha ya wengi kuonesha nia ya kupata mafunzo hayo.
"Tangu Shule ilipoanzishwa tumeshatoa mafunzo zaidi ya 60 na wahitimu 14,000 Shule ya Mwalimu Julius Nyerere inamilikiwa na Vyama sita rafiki vilivyopo Kusini Mwa Afrika ambavyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), MPLA, SWAPO, ZANU PF, ANC na FRELIMO na mdhamini wake mkuu ni Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).


0 Comments