TAKUKURU PWANI YAOKOA ZAIDI YA MIL .300 ZILIZOPOTEA KUPITIA AKAUNTI FEKI YA KIJIJI CHA MSUFINI

TAKUKURU  Mkoa  wa Pwani  katika  kipindi  cha Januari  hadi  Machi  2025 ilifanikiwa  kuokoa mapato  ya  asilimia 10% ya mauzo  ya ardhi  ya Halmashauri  ya Kijiji cha Msufini Kidete Wilayani  Mkuranga Mkoani Pwani fedha hizo ziliwekwa kwenye  akaunti feki  ya kijiji  hicho  iliyoghushiwa  na mwanasheria  wa Kampuni iliyouziwa  eneo la kijiji.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa  TAKUKURU Mkoa wa Pwani Domina  Mukama alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano ulipofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisini kwake leo tarehe 29 Mei 2025.
"Halmashauri ya Kijiji ilitakiwa  kulipwa  Mil. 385 kama asilimia 10% ya mauzo , ambapo  fedha  hizo ziliwekwa  kwenye  akaunti  feki  yenye  jina  kama  la  akaunti  ya Kijiji  iliyowasilishwa na Mwanasheria  wa  Kampuni hiyo " amesema Kamanda  Mukama.
Aidha Kamanda ameitaja  jina la Kampuni  hiyo kuwa ni Brilliant Sanitary  Ware  Company Limited ilifanyika  malipo  ya kiasi  Mil.385  wakiamini  kuwa  wanalipa  ushuru  wa Kijiji  cha Msufini  katika  akaunti  halali ya Kijiji na kumbe  ilikuwa  ni akaunti  ya  Mwanasheria.
Aidha  baada ya  kufanyika malipo  Mwanasheria  huyo  alizitoa  fedha  zote  na kuzifanyia  matumizi binafsi.
TAKUKURU imefanmikiwa  kurejesha  fedha  zote Mil.385 serikalini  kupitia  Halmashauri ya Kijiji cha Msufini, na tayari  fedha  hizo  zimepangiwa matumizi ya kujenga  jumla  ya madarasa mawili  ya Shule  ya Sekondari  Mbezi Gogoni  na madarasa  mawili  katika Shule ya Msufini.
"Pia  fedha hizo zimejenga nyumba mbili  za waalimu , wamechimba matundu 12 ya vyoo  kisima kirefu cha maji  na ukarabati  wa Zahanati  Kijiji cha Msufini" amesema Kamanda Mukama.
Kamanda Mukama amesema kuwa  katika  kipindi  tajwa  ofisi  ilifanya  chambuzi  za  mfumo  14 ikiwa ni pamoja na  eneo  la makadirio  ya ukusanyaji  wa mapato m katika Halmashauri  ya Mji Kibaha , Mafia na Kituo cha utalii Kazimzumbwi.Katika  chambuzi wa  mfumo  wa usambazaji  maji  uliofanyika  kuna mapungufu  yalibainika  na hatua  zilichukuliwa.
 Kamanda Mukama amesema  TAKUKURU Pwani  imefuatilia  utekelezaji  wa miradi  ya maendeleo  338 yenye  thamani  ya zaidi  ya Bi. 18 na utekelezaji wake unarizisha.
 Amesema kuwa  kwa upande wa uelimu kwa umma  TAKUKURU  imewafikia  wananchi  wa makundi  mbalimbali  ili waweze  kuiunga  serikali  mkono  katika kuzuia   vitendo  vya rushwa  kwa kupitia  semina 67, mikutano  ya hadhara 72, vipindi vya redio 5 na uimarishaji  Klabu za Wapinga  rushwa 130.
"Kesi 10 zimeamuliwa  ambapo  Jamhuri  
 imeshinda kesi zote na jumla ya kesi 23 zinzendelea Mahakamani" amesema Kamanda Mukama.

Wakati huohuo Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Mukama amesema kuwa wako kazini katika kipindi cha kulekea uchaguzi mkuu ujao katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa kwa kuwafikia wadau wote ambao ni vyama vya siasa , wasimamizi wa uchaguzi , wanahabari, wananchi na jamii nzima kwa ujumla .
"TAKUKURU Pwani ninaasa wananchi kufuata sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuwa salama na kuepuka migogoro yenye kuleta viashiria vya rushwa" amesema Kamanda Mukama.

Post a Comment

0 Comments