SPIKA WA BUNGE DKT. TULIA ACKSON AASA WANAOJIPITISHA KABLA YA WAKATI

 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Ajira na watu Wenye ulemavu  Ridhiwani  Kikwete akisalimiana na wajumbe nje ya ukumbi huo leo Tarehe 25 ,Aprili 2025. 

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (MB) amewataka viongozi  hao kutobabaishwa na wanaopitapita kutafuta nafasi za uongozi kabla ya muda badala yake wawapuuze.

 Dkt. Akson amesema uongozi hautafutwi kwa nguvu bali unapangwa na Mwenyezi Mungu

Wakati huohuo Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Mkoa wa Pwani  Lailah Burhan Ngozi Mkoani Pwani ambaye alikua  mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kibaha Mjini wakati   Mbunge wa Jimbo  Silvestry Koka  alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi  ya mwaka 2020 - 2025. 

Ngozi amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan   ameshirikiana vema na wabunge katika kuleta maendeleo na kumpongeza Mbunge  Koka kwa kazi kubwa kwa kuutumia uongozi wake kwa maslahi mapana ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

" Tunahitaji Viongozi bora kwa kuzingatia misingi bora ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo inatoa majibu ya kuifanya  iendelee kuwa Chama Kiongozi."amesema Ngozi.

Amesema kuwa  CCM siyo  chama goigoi bali ni chama chenye uwezo wa  kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.

 Ngozi amesema kuwa  wanaopinga maendeleo yaliyofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan hawana sera hivyo wasiwapotezee muda.

"Msitafute wagombea wababaishaji nje ya CCM tafuteni  viongozi wanaotokana na CCM kwani wao wamelelewa na wana maadili ya Kiuongozi." amesema Ngozi.

Amehitimisha kwa kuwataka viongozi wa mkutano huo kutosemeana maneno mabaya hususani kwa  viongozi walioko madarakani.

Kutoka  kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge wakiteta jambo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa  kupitia Kundi la Wazazi  y Chama Cha Mapinduzi  MNEC Hamoud  Jumaa.

Post a Comment

0 Comments