CHATANDA ACHAGIZA WANAWAKE KUJITOSA UCHAGUZI MKUU 2025



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama Cha Mapinduzi  Tanzania (UWT ) Mary Chatanda  pichani juu ametoa rai kwa wanawake wote  nchini kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea katika ngazi za Udiwani na Ubunge  kwenye uchaguzi mkuu ujao hukulengo likiwa  kumpa ushindi wa kishindo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi  hivyo nawaomba  wanawake mjitokeze  kwa wingi  katika kugombea  nafasi  za Udiwani na Ubunge  lakini pia  kujipanga kumuunga   mkono  mwanamke mwenzetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan twendeni tukavunje rekodi  ya kumchagua  Rais mwanamke kwa mara ya  kwanza nchini  na kumchagua kwa  kura ningi  ndani ya boxi" amesema Chatanda.

"Katika kufanikisha ushindi huu wa kishindo kila mmoja wenu ahakikishe  yumo  katika daftari la wapigakura 2025 shime kwa ambao bado  hawajajiandikisha wajitokeze  kwenye zoezi la uandikishaji kwenye Daftari  la mpiga kura. itikadi za vyama  nitasimama kidedea anashinda hivyo ingieni kwenye majimbo kwa kifua mbele mimi nitapanda juu ya meza  kuhakikisha majina yenu yanarudi" amsesema Mwenyekiti wa UWT Chatanda.

Chatanda amesema hayo jana usiku tarehe 22 Machi 2025 alipokuwa mgeni rasmi  kwenye hafla ya usiku wa  Huba Huru Gala iliyokua na kaulimbniu isemayo 'Acha Upendo Utawale' iliyofanyika  kwenye Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es Salaam.

Chatanda amesema kuwa anawapongeza uongozi wa  Clouds  Media Group na heshima za kipekee ziende kwa Mkurugenzi  Mtendaji  wake Joseph Kusaga kwa kumualika kuwa mgeni rasmi sambamba na kufanikisha hafla hiyo.

"Nawapongeza sana CMG kwa kuendelea kuwa wabunifu  wa kuandaa hafla mbalimbali  nchini na zenye  mlengo  wa kujenga  zaidi  kizazi  cha wanawake  hasa kiuchumi,kifikra na kijamii" amesema Mwenyekiti huyo.

"Leo ni siku ya kipekee tena ikiwa  ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa ndugu zetu waislam na  pamoja na  wakristu  ambao wako kwenye mfungo wa Kwaresma  wote tumekutana hapa  siyo tu  kwa sherehe  bali kwa  dhamira  thabiti  ya kuweka  ahadi mpya  kwa mustakali  wa wanawake  wa Tanzania.

"Hafla hii imelenga kutukutanisha wanawake   kutoka kada mbalimbali bila kujali itikadi za vyama,dini ,rangi zetu na makabila yetu imekuja wakati sahihi  kwani  sote tunatambua  kuwa wanawake  ni Jeshi kubwa  na kwa hapa nchini tuko wengi zaidi kuliko wanaume  kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya watu na makazi  ya mwaka 2022 takriban asilimia 51 ya watanzania  ni wanawake" amesema Chatanda.

Amesema kuwa "Tunasimama  hapa  kama wawakilishi wa kizazi  cha sasa  cha  wanawake  tukiwa na dhamana  ya kuwaongoza  dada, binti na mama zetu  kuelekea  kwenye umoja thabiti  wa maendeleo  na ustawi wa jamii  yetu  kwa ujumla.

"Usiku huu ni usiku wa  mabadiliko tumekusanyika  hapa siyo kwa burudani tu  bali kwa sababu ya  kutimiza  jukumu kubwa  tulilonalo kama wanawake  wa taifa hili  kwani kuna  msemo usemao ukiwawezesha wanawake  umestawisha taifa"  amesema Chatanda.

"Tunahitaji kukomesha dhana potofu  kuwa adui  wa mwanamke  ni mwanamke kauli hii haijawahi kuwa kweli  na leo  tunathibitisha  kuwa sisi ni nguzo ya maendeleo siyo maadui  wa maendeleo baina yetu na sasa rafiki wa mwanamke  ni mwanamke mwenziye tukishirikiana , tukisaidiana na tukiamini katika uwezo  wetu hakuna  linalotushinda"
amesema Mwenyekiti huyo .

"Historia imethibitishwa   kuwa pale  ambapo  wanawake  wameungana  maendeleo  yamekuwa dhahiri na mshikamano wetu ndiyo unajenga nguvu ya jamii ".

"Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  ametimiza miaka minne  tangu ailipoingia madarakani  tumeshuhudia  akipongezwa  kila kona ya  nchi hii  na shuhuda  mbalimbali  za kazi  kubwa  na  nzuri iliyofanyika  katika  kipindi  hiki , Rais  wetu ametuheshimisha  wanawake wa nchi hii, Bara la Afrika na ulimwengu kwa ujumla kwa kupitia  aina ya uongozi wake  unaozingatia 4R na sisi ni mashuhuda hapa mara  tatu mfululizo ametajwa kuwa miongoni mwa wanawake100  duniani wenye ushawishi, amepata tunzo nyingi ndani na nje ya nchi hakika  amekuwa kinara  wa mageuzi makubwa katika  kujenga  kizazi chenye usawa wa kijinsia nchini kwetu"amesema Chatanda.

"Baadhi ya  juhudi zake  ni pamoja na  kuanzisha mfuko wa maendeleo ya Wanawake (WDF) ambao  umewezesha  wanawake wengi kupata  mitaji ya biashara, mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri isiyo na riba  kwa makundi ya  wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambayo imesaidia  makundi haya hasa katika ngazi za vijiji, kata  kupata uwezeshaji, kuwezesha makundi  maalum  wakiwemo wamachinga kutambulika kuwajengea miundombinu kuwatafutia  fursa za  kibenki na  zenye riba nafuu" amesema Chatanda.

"Amewawezesha wasanii kupata mfuko wa kuwakopesha na kuwatafutia fursa mbalimbali nje ya nchi mfano ziara  yake  aliyofanya nchini Korea, kuimaarisha sekta  ya afya ya uzazi  kwa kuhakikisha huduma  bora za mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi zaidi kupitia ujenzi  wa  miundombinu  ya sekta  ya Afya na uwepo  wa vifaa  tiba  vya kisasa hali iliyopelekea  kupunguza vifo vya wanawake wajawazito mama kutoka  556 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2020 hadi vifo 104 kwa vizazi  hai 100,000 na kwa upande wa  watoto wachanga  vifo vimepungua  kutoka vifo 67 kati ya vizazi 1,000 hadi 43 kwa vizazi   hai 1,000 na matokeo haya yamemwezesha Rais wetu  kutunukiwa  Tunzo ya Goal Keeper Award " amesema Chatanda.

"Tunzo hii ni heshima  kwa wanawake waliovunja  mipaka  na kufanikisha  maendeleo makubwa  katika jamii zetu tuendelee  kusherehekea, kuthamini na kuenzi  mchango  wa wanawake wa Tanzania" amesema Chatanda.

Aidha Chatanda ametoa pongezi kwa  Kampuni ya   Clouds Media Group kuwa wameandika  historia  Barani Afrika  kuwa na Redio  ya Wanawake  pekee inayofahamika kwa jina la  Malkia Choice FM inayoongozwa na  Mkurugenzi  Mtendaji Juhaina Kusaga, kuwa  imedhihirisha  dhamira ya kweli  ya Clouds  Media Group katika kuendeleza  usawa wa kijinsia  na kuwa  sauti ya wanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Hafla hiyo ya Usiku wa wa Huba Huru imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni Rehema Kyando kutoka Benki  Kuu ya Tanzania (BOT) ambapo amewaasa wanawake kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwa kujiwekea akiba na kukuza  mitaji na kuacha kununua vitu vya anasa.

Wengine waliohudhuria ni viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga , Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Mgalu wanawake wasanii kutoka vikundi mbalimbali huku wafanyabiashara Jiji la Dar es Salaam wamemchangia Rais DKT.Samia Suluhu Hassan kiasi cha Mil.700 kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments