Hajji ambaye ni mtoto wa kiungo mahiri wa Yanga, Pan African
na Taifa Stars, alianza maneno yake
yaliyoanza kuamsha walio msibani kumsogelea kwa kusema atamuagiza mdogo wake
Jerry aende Morogoro kumwakilisha kwenye
mazishi na klabu ya Simba itatoa ubani
wa kiasi cha sh. 500,000, ambazo Murro atakwenda kuzikabidhi kwa familia.
“Niko hapa kwa niaba ya Rais wa Klabu ya Simba Evans
Aveva , hivyo kwa niaba yake na
wanachama wa Simba tumekumbwa na msiba mzito
hivyo hakuna jambo jingine la
kusema bali ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu na ampumzishe kwa amani” alisema Manara.
Aidha aliwavunja mbavu zaidi
mamia ya watu waliokuwa msibani baada ya kusema kwamba anamjua mdogowake
Jerry Murro kwa kupenda kwake sifa na ushindani akija atatangaza kiasi kikubwa
zaidi ya kile kilichotolewa na Simba.
Murro ambaye alikuwepo msibani mapema kabisa, alianza kwa
kusema “kwa niaba ya ya Rais , wanachama
, wapenzi wa Klabu ya Yanga,ningependa
kuwafahamisha kwamba mume wa Eliza ni
shabiki na mwanachama wa klabu yetu ya Yanga,
hivyo mbali ya kumpoteza mwanahabari mwenzetu lakini pia tumempoteza shemeji”
Murro aliendelea kwa kusema kuwa Eliza alikuwa kiungo muhimu
na sisi wana Yanga tunatambua na
kuuthamini mchango alioutoa kwa klabu
yetu ila kulikuwa na siri moja ambayo
ilimpa wakati mgumu sana marehemu katika
enzi za uhai wake ndani ya miaka minne iliyopita, kwani alilazimika kuandika
habari za klabu ya Yanga ambao walikuwa
wakiongoza katika ligi ya mabingwa licha
ya yeye kuwa shabiki na mwanachama mnazi
wa Simba.
“Elizabeth alilazimika kuandika habari zetu jinsi
tulivyokuwa tuking’ara huku huku wenzetu
wa matopeni wakiwa wamekwama, sisi Yanga tutatoa
ubani wa sh. 500,000 pia
tutafanya kama alivyoniagiza
Manara nitaungana wafiwa kwenda kuiwakilisha Simba kwenye mazishi ya marehemu Mkoani Morogoro ” alisema Muro
na kuamsha kicheko kwa wawili hao walipokuwa wamezungumzwa na waombolezaji
ambao idadi yao kubwa ni wanahabari wa vyombo
mbalimbali.
Murro alisisitiza kwamba yeye bado ni Msemaji halali wa
Yanga kwa sababu bado hajapata barua
rasmi ya kusimamishwa kwake kutoka
Shirikisho la Soka nchini (TFF), na kwamba anaripoti kwa mwajiri wake Yanga
kama ilivyo ajira yake inavyomtaka.
Wakizungumza katika nyakati tofauti ,Manara alikiri kwa
kusema kuwa Klabu ya Simba imempoteza
mwandishi habari mahiri ambaye pia alikuwa mwanachama mwenye kadi ya klabu hiyo. Manara
alijiongeza zaidi na kusema pamoja na kwamba wanataniana na Yanga, lakini
amezisikia habari za Murro kumtafutia pesa za matibabu kwa mashabiki wa Yanga
na kusema ni uungwana unaopaswa kuendeleza na si vinginevyo.
“Ameniambia mdogo wangu Murro wameshafikisha milioni na bado
wanachanga, kiukweli huyu dogo ni muungwana, nasubiri atomize ahadi yake,
nitazipokea, sisi ni watani na si wagomvi” alisema Manara.
Mbali ya wasemaji hao, nae Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi
wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto alitoa salamu
za rambirambi chama hicho na kusema kuwa
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mwenzetu ambaye ni
mwanachama wetu”.
“Mchango wake bado ulikuwa unahitajika , alikuwa mcheshi
alijitoa katika kazi zake za kila siku kwa hali na mali binafsi nilimfahamu vema namna alivyokuwa akijituma ipasavyo TASWA inatoa pole kwa familia na wanatasnia kwa ujumla kwa kuondokewa na mpendwa wao kifo hakizuiliki lakini tuna wajibu wa kumuombea mwenzetu na sisi tunatoa rambirambi
kiasi cha sh.500,000” alimalizia Pinto.
Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire alisema kuwa
ametumwa kumwalisha Kanali Charles Mbuge
kutoa salamu za rambirambi kiasi cha 300,000 kwa niaba ya timu yao. Miongoni mwa wa soka waliofika kwenye
msiba huo ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa Dar Es Salaam, Almas
Kasongo Mwenyekiti wa Kamati ya soka la
vijana, Ayoub Nyenzi na Wachezaji wa
zamani Ken Mkapa, Mohemed Hussein
Mmachinga na Ramadhan Kampira.
Marehemu Mayemba alizaliwa
Desemba 1980 alikuwa Kaimu Mhariri
Msaidizi wa wa Michezo na Burudani
Katika Kampuni ya Business Times Limited wachapishaji wa gazeti la Majira .
Mayemba alifariki Jumamosi iliyopita saa mbili usiku baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake Tabata Kisukuru na alifariki dunia wakati akiwahishwa Hospitali ya Rufaa
ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Marehemu ameacha mume na watoto watatu pia atazikwa leo kwenye makaburi ya Kola
Mkoani Morogoro. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.
0 Comments