MWILI WA MAREHEMU ASHA BAKARI WAWASILI ZANZIBAR , MAZISHI LEO SAA NNE ASUBUHI ZANZIBAR

Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na mwili wa marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitoka  kwenye matibabu nchini India.

Marehemu atazikwa leo  katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi . 
Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi  leo  saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu jana.
Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar jana  jioni
Mwili wa Marehemu ukishushwa katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar. 
Wananchi wakiupokea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa Uwanja  jana jioni.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho na Viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiuombea dua mwili wa marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Zanzibar  jana  jioni tayari kwa mazishi leo  saa nne asubuhi katika kijiji cha kiyanga. 

Ndugu na Jamaa wakiwa na huzuni baada ya kuupokea mwili wa marehemu jana  jioni 



Wananchi wakishiriki katika kuombeleza msiba wa marehemu Asha Bakari Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar aliyefariki Nchini Dubain wakati akitokea nchini India katika matibabu.
Ndugu na Jamaa na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuombea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili nyumbani kwa  kaka wa marehemu jana  kwa ajili ya matayarisho ya mazishi leo katika mtaa wa Jang'ombe  
Waombolezaji wakiwa katika msiba jangombe kwa ndugu wa marehemu wakisubiri taratibu za mazishi leo saa nne asubuhi.
Ndugu wa marehemu wakiomboleza msiba wa ndugu yao nyumbani kwaoJang'ombe Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud akizungumza na Ndugu wa c na marehemu baada ya kuwasili kwa mwili  jana Jang'ombe kwa nduga zake kwa mazishi leo
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com

Post a Comment

0 Comments