FEDHA , MKESHA WA AMANI KUOKOA VIFO VYWA WAJAWAZITO NA WATOTO


Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste,(Katikati)  ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu  Godfrey  Malassy  alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
Na  Skolastika Tweneshe-MAELEZO

Fedha zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea amani  nchini zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji  hasa afya ya mama na mtoto.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu  Godfrey  Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Malassy alisema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua vifaa vinavyotumia nishati ya jua (solar Panels) ili kuwasaidi wamama wajawazito na watoto wanaozaliwa.

“Kina mama wajawazito na watoto wanakufa mahospitalini kutokana  na kukosa umeme hasa vijijini,  hivyo tumeamua fedha zitakazopatikana mkesha huu tutanunua solar” alisema Malassy

Aidha Askofu Malassy  amewaomba wananchi   kuzidi kumuombea Rais John Magufuli katika kuliongoza Taifa la Tanzania ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi ambayo tayari imekubalika ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti huyo alitambulisha kitabu  kiitwacho IJUE  SIRI YA AMANI  KWA  TAIFA ambacho kinauzwa Sh.5000 amesema kuwa  kitabu hicho kina lengo la kuelimisha thamani na jukumu la watanzania kuilinda Amani  bila kujali itikadi za  dini, siasa wala ukabila

Pia ameomba kwa atakaeguswa na  matatizo yanayowakumba wamama wajawazito anaweza kutuma mchango wake kwa namba zifuatazo 0755202204,0719202204,0684202204.

Mkesha huo  ni wa 18 tangu uanze kufanyika  na mwaka huu utafanyika  katika Uwanja wa Uhuru usiku wa tarehe 31 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Awamu ya Tano Mhe.  John Pombe Magufuli.

Post a Comment

0 Comments