WHO YATOA DAWA ZA MILIONI 42.2 ILI KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU NCHINI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Donan Mmbando (katikati) akipokea msaada wa dawa za kuthibiti maambukizi ya kipindupindu kutoka kwa mwakilishi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Rufaro Chatora(kulia). Kushoto ni Mganga Mkuu kutoka Wizara hiyo Dkt. Margaret Mhando
  Na Ally Daud-MAELEZO

Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imepokea msaada wa dawa za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini kutoka Shirika la Afya Duniani zenye thamani ya shilingi milioni 42.2.

Msaada huo umepokelewa leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Donan Mmbando.

Akizungumza mada baada ya kupata msaada huo amesema dawa hizo ambazo ni katoni 1000 za water guard, lita 100 za Cresol Saponated zitasaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Naye mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) nchini Tanzania Dkt.. Rufaro Chatora amesema kuwa ni wajibu wao kusaidia kupamabana na maambukizi ya ugonjwa huo ili kuhakikisha unatokomea nchini.
Ameongeza kuwa ni jukumu la wananchi la kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kudhibiti hali ya usafi kuanzia mwili , chakula na mazingira yanayowazunguka kwa ujumla.

Dkt. Chatora amesema kuwa ni vema wananchi wakapigwa marufuku kuuza vyakula sehemu za kampeni ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha , Mwakilishi huyo wa WHO amesema kuwa Shirika lake litatoa msaada wa shilingi milioni 159.8 kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kuzuia ugonjwa wa KipindupinduNchini .

Post a Comment

0 Comments