MAADHIMISHO YA WIKI NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAFANYIKA TEMEKE JIJI DAR ES SALAAM (ENDESHA SALAMA-OKOA MAISHA)

Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel akuzungumza na wananchi juu ya Kuzuia kabisa mwendo kasi kwa magari makubwa barabara ya kutoka bandarini kuelekea ubungo kupitia ama Barabara ya Kilwa ama ile ya Mandela kwa wakati wote, na kuweka msisitizo wa alama za mwendo kasi katika barabara hizo kwakuwa pia imekuwa ikichangia kukosa umadhubuti wa breki pindi tatizo la ghafla linapojitokeza,  jana jiji Dar Salaam.

Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi Ambaye ni Mkurugenzi wa Kmpuni ya A&T Brothers co.Ltd Abdulmalik Mollel jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
Wanafunzi wakitoa maelekezo kwa wananchi jinsi ya kutumia vifaa maalum vya kuzuia magari ili watembea kwa miguu wavuke barabara jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usala ma Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
 
Mrakibu wa Jeshi la Polisi Chang'ombe Temeke akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupungua kwa ajali kwa kiasi kikubwa katika Manispa ya Temeke jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya Dar es Salaam.
 Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke Thabit Massa akizungumza na waandishi wa habari juu ya wananchi kutunza miundo mbinu ya barabara jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel (mwenye suti nyeusi) akiwa pamoja na  Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke Thabit Massa wakipatiwa maelekezo na wanafunzi sehemu za makutano ya barabara zinazosababisha ajali  jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya Dar es Salaam.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A&T Brothers Co. Ltd Abdulmalik Mollel akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi jana katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam.
 Mgeni Rasmi Ambaye ni Mkurugenzi wa Kmpuni ya A&T Brothers co.Ltd Abdulmalik Mollel na Kaimu Mwenyekiti Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke akianga marabaada maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabara Kanda ya Dar es Salaam Picha na Emmanuel Massaka.
---
HOTUBA YA MGENI RASMI UFUNGUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOA WA KIPOLISI WA TEMEKE. TAREHE 26/8/2015
Ndugu; - Mkuu wa police Trafic mkoa wa Temeke (RTO). - Mwenyekiti usalama barabarani ndugu -Thabit - Mkuu wa Operesheni – Temeke , Mr Mchuya - Mkuu F.F.U – Mkoa polisi – Temeke - Ndugu kombe – mkuu wa kituo cha polisi- Chang`ombe - Viongozi mbalimbali wa kipolisi mkoa wa Temeke - Waalimu na wanafunzi wote mliohudhuria - Wadau wote mliohudhuria, mabibi na mabwana – Itifaki imezingatiwa 

Baada ya kusikiliza na kuelewa kwa umakini changamoto mbalimbali zilizotolewa na baraza la watoto la usalama mkoa wa Temeke, pia wadau wa usalama barabarani ,yafuatayo naomba kuyarejea ili tuweze kuyapatia ufumbuzi wa mara moja kulingana na uwezo wangu na kwa ushirikiano wa Polisi mkoa huu na wadau wote kwa ujumla; Changamoto zinazosababisha kurudisha nyuma jitihada za kupunguza ajali ni pamoja na zifuatazo:
1. Kutokuwa makini kwa madereva waendeshao vifaa vya moto
2. Kutokuwa na elimu ya kutosha ya alama za barabarani kwa watumiaji ambao ni waenda kwa miguu au waendesha vyombo vya barabarani
3. Kutofuata alama za barabarani kwa watumiaji kama itakiwavyo
4. Wasimamizi wa usalama barabarani kutokuwa makini hasa hatua zinapotakiwa kuchukuliwa mara moja. Ndugu viongozi na wadau wote wa usalama mkoa huu na Taifa kwa ujumla, Rekodi zinajionyesha ni kwa jinsi gani tunavyopoteza ndugu na jamaa zetu kwa sababu ambazo zinazuilika,ikizingatiwa kuwa hawa tunaowapoteza kwa ajali hizi ni moja ya nguvu kazi ya Taifa hili.
Na wadau wameomba serikali iweze kuchukua nafasi ya kupunguza ajali hizi kwa kunusuru maisha ya watu, na hasa ikizingatiwa kauli mbiu ya mwaka huu “ENDESHA SALAMA- OKOA MAISHA”.
Ndugu wageni waalikwa, viongozi mbalimbali wa kipolisi,wanafunzi, waalimu na waandishi wa habari, Ikumbukwe kuwa serikali ni sisi tulioko hapa kwa kuwa ndio Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa nchi hii amewaamini viongozi hawa walioko hapa kusimamia jukumu hili maalumu la usalama mkoa huu wa Temeke. 
Sina hofu kabisa na (RTO) wa Mkoa huu, kwani Temeke imepunguza ajali kwa asilimia hamsini (50%) kutoka 2014/2015 na hii inaonyesha jitihada na mikakati madhubuti inayofanywa kama ambavyo chati imeonesha, Nami kwa nafasi yangu kama mgeni rasmi leo, pia nikiwa mdau mkuu wa usafirishaji, ninashauri viongozi wafanye yafuatayo,ikiwa pia nitakuwa mstari wa mbele ktk kuhamasisha sekta binafsi zinazonihusu ili malengo yetu kwa pamoja yaweze kufikiwa;
1. Elimu itolewe mashuleni: Kikao cha wakuu wa shule, Afisa Elimu, Polisi na wadau wengine kiitishwe mara moja, ili yapitishwe maazimio ya elimu hii ya usalama barabarani, iwe ni yenye kutolewa kwa muendelezo katika kipindi chao wawapo masomoni.
2. Kiitishwe kikao cha wadau wa usafirishaji, viwanda,na watumiao vyombo hivi vya moto watokao ktk eneo la kimkoa kipolisi Temeke, ili washiriki katika kuchangia elimu hii kwa gharama za vitabu vyenye masomo hayo vipatikane kwa wanafunzi.
3. Vipindi vya siku za mpira uwanja wa Taifa: ninashauri muda wa kuanzia jioni saa moja, magari yote yaliyoharibika njiani yasiachwe kabisa bila kutolewa barabarani, 
kwani waendesha pikipiki huwa wanashindwa kuyaona kwa wakati na kusababisha ajali zisizo na sababu na kuongezeka kwa vifo vya Raia wasiokuwa na hatia.
4. Elimu katika makundi maalum: Iendelee kutolewa na kuthibitishwa kwa vyeti hasa waendesha bodaboda na magari makubwa.
5. Mwendo Kasi:Kuzuia kabisa mwendo kasi kwa magari makubwa barabara ya kutoka bandarini kuelekea ubungo kupitia ama Barabara ya Kilwa ama ile ya Mandela kwa wakati wote,na kuweka msisitizo wa alama za mwendo kasi katika barabara hizo kwakuwa pia imekuwa ikichangia kukosa umadhubuti wa breki pindi tatizo la ghafla linapojitokeza,hivyo kupelekea ajali kutoepukika.
6. BREAKDOWN: Magari ya Breakdown yatumike kutoka polisi kwa zile gari ambazo zitakuwa zimepata matatizo ya kiufundi,na kusababisha uhatarishaji wa ajali kutokea,ziweze kuvutwa na kuwekwa nje ya eneo hatarishi na hasa vipindi vya usiku unapokuwa umeingia. Mwisho ninawashukuru wageni waalikwa, wadau wote waliowezakuitikia wito wa kongamano hili,na sasa ninatamka Rasmi’ Kongamano la Wiki ya Nenda Kwa Usalama limefunguliwa.’
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Temeke, ENDESHA SALAMA-OKOA MAISHA!! 
Ni kwa ujenzi wa Taifa; Ndg. ABDULMALIK S. MOLLEL MGENI RASMI. A&T BROTHERS TRANSPORT CO.LTD

Post a Comment

0 Comments