PROMOSHENI YA MULTICHOICE ,KINGAMUZI KIPYA KUFIKA TAMATI JUMAPILI


KAMPUNI ya Multichoice Tanzania tawi la hapa nchini wametangaza mwisho wa promosheni ya king’amuzi kipya itafanyika Jumapili katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Uhusiano wa Multichoice, Barbara Kambogi, alisema wamezindua king’amuzi hicho ambacho kiliuzwa kwa bei ya chini wakati wa kombe hilo ili kutoa fursa kwa wadau wa michezo nchini kuweza kuona mechi zilizokuwa zikiendelea barani Afrika.

Naye Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu, alisema kwamba bei ya king’amuzi hicho ni sh. 99,000 kwa wateja wapya na wale wa zamani wanaweza kubadilisha kwa sh. 39,000 na promosheni hiyo ni ya muda mfupi, ambako itafikia tamati Jumapili siku ya fainali.

Aidha, alisema pia wamezindua rasmi king’amuzi kipya cha Dstv HD, dikoda ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Naye Meneja Mwendeshaji wa Multichoice, Baraka Shelukindo, alisema king’amuzi hicho kipya kabisa kitakuwa na uwezo wa hali ya juu, ambapo kitakuwa kinaonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi ikiwa ni pamoja na sauti ‘Dolby Digital 5.1’.
 

Post a Comment

0 Comments