Meneja
msaidizi wa Castle lite Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam juu ya kupatikana kwa washindi wa shindano la bia ya
castle lite Yatch party ambapo jumla ya washindi kumi na tano nchi nzima
wamepatikana .Pembeni yake ni meneja wa bia ya Castle lite Geofrey Makau.
JUMLA
ya washindi 15 wa shindano la Castle lite Yatch Party wamepatikana jleo asubuhi na wanatarajiwa kuwasili jijini Dar Es Salaam
muda wowote kwa ajili ya Tamasha kubwa la ndani ya bahari litakaloendeshwa na
Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia bia yake ya Castle Lite.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam
Meneja msaidizi wa bia hiyo Victoria Kimaro alisema kampeni ya kuwasaka
washindi hao ilichukua takribani miezi mitatu ambapo iliendeshwa kwa mikoa mine tu nchini.
Bia
ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
leo imefunga rasmi promosheni ya ‘Lite Up The Weekend’ ambayo imeendeshwa kwa
muda wa miezi mitatu katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam.
Alisema kwa kupitia bia hiyo waliweza kufanya
promosheni huku lengo kuu lilikuwa ni kuwazawadia wateja wake na watanzania
kwaujumla na kuwakutanisha pamoja na kufurahia kwa kuweza kusherekea kwa
kushiriki katika tamashi hilo kubwa litakalofanyika katikati ya bahari ya Hindi
sanjari na burudani mbalimbali zitakazokuwepo.
Makau
aliwapongeza washindi hao na kuwataka kwenda kuwa mabalozi wazuri wa bia ya
Castle Lite popote waendapo huku wakizingatia kwamba hii ndiyo bia pekee kuweza
kuendesha shindano la kipekee kwa kuwashindanisha kistarabu wateja wake na
hatimae kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu na kuhudhuria katika hili
tamasha la kipekee.
Makau
aliwataja washindi hao waliopatikana jana kuwa ni Issack Mngara, Josephine
Nateya, Woinde Shizza, Salum Abdallah, Andoline
Mwakyonde na Sunday Maximillian.
Washindi
wengine ni Maneno Frank, Tumaniel Moshi, YuvenalGilson, Hellone Misso, Samson
Mwikwabe, Martin Lyanga, Sunday Magembe na John Bosco Mushi.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari leo asubuhi Meneja Makau alisema anatoa
pongezi kwa wote kutokana na kufikia tamati ya promosheni hii na kuwapongeza washindi waliopatokana katika
droo kubwa nay a mwisho ya kampeni hii .
Washindi hao
pamoja na wenzi wao watapata fursa ya
kufurahia wikiendi yao kwa kupitia Castle Lite huku wakilipiwa
gharama za usafiri , hoteli chakula cha jioni
na burudani katika Bar ya kifahari Jijini Dar es Salaam kadhalika washindi hao
watazungushwa huku wakiwa ndani ya
boti ambako kutafanyika pati kubwa na ya aina yake huku wakiburudika kwa muziki
na mwisho watashushwa kwenye sherehe
ya kumalizia wikiendi ya VIP na Casltle
Lite.
Aidha
amewashukuru watanzania wote kwa kujitokeza
kushiriki kwa wingi kwenye promosheni
hii iliyofanyika kwa muda wa miezi
mitatu.
0 Comments