muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Daktari Bingwa
Edward Schaeffer kutokaHospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya
kufanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita
baada ya
kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali
ya Rais
Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa
mapumzikoni
akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa,
kabla ya
kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea
kufanya
mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea
salamu za
Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe
ya dunia
pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa
viongozi
mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje.
Naye
amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward
Schaeffer
muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo
alifanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hali ya
Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na
kuwa
mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa
nyuzi siku
chache zijazo.(Picha na Freddy Maro)
0 Comments