Profesa
Nkoma alisema kuwa iwapo
wamiliki wa Blogs nchini wataanzisha
chama chao upo
uwezekano mkubwa wa TCRA kuwasaidia mchakato huo na pia kuendelea kuungana na chama hicho
kwa kuendelea kutoa elimu zaidi.
Mbali
ya kuwataka kuanzisha
chama hicho bado
aliwataka wamiliki wa blogs
nchini kuendelea kuifanya kazi
hiyo kwa kuheshimu misingi ya
maadili .
Pia alisema kuwa
TCRA wataendelea kuwa na mkakati wa
kuendelea kutoa elimu na kukutana na wamiliki wa Blogs ili kukumbushana maadili zaidi.
Akielezea kuhusu uwajibikaji wa blogs nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 alitaka kuhakikisha
wanatoa nafasi sawa kwa vyama
na wagombea wote
bila upendeleo.
0 Comments