Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema
Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti
Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa
insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo
kusini mwa Afrika(SADC).Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati
wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC
unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe
ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia
nchi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu
na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda
mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika
katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe
leo.Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na Dkt Stergomena Tax [katibu mkuu wa SADC] na kwa upande wake wa kushoto ni Nkosazana Dlamini-Zuma (Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika)
Mtoto
wa Kitanzania, msichana Neema Steven Mtwanga, ameibuka kinara katika
Mashindano ya Utunzi wa Insha katika nchi wanachama wa Jumuia ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kushika nafasi ya kwanza
miongoni mwa washindani 39 waliowania Tuzo ya Utunzi wa Insha hiyo kwa
Mwaka 2014.
Msichana
Neema Steven Mtwanga, 16, kutoka Shule ya Sekondari ya Naboti, Mkoa wa
Njombe, ametunukiwa Tuzo ya ushindi huo katika Mkutano wa 34 wa Kawaida
wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC ulioanza leo katika Hoteli ya
Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe.
Nafasi
ya pili imeshikwa na Kudzai Ncube kutoka Shule ya Sekondari ya Mazowe
nchini Zimbabwe na nafasi ya tatu imeshikwa na Manxoba Msibi kutoka
Shule ya Sekondari ya Etjendlovu katika Swaziland.
Kwa
ushindi huo, Neema Steven Mtwanga ambaye yuko kidato cha nne,
amezawadiwa hundi ya dola za Marekani 1500 ambayo ni sawa na shilingi
milioni 2.3 na amelipiwa gharama zote za kumwezesha kushiriki katika
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC na kukabidhiwa zawadi hiyo. Aidha,
Neema amepewa zawadi ya ipad kwa ajili ya matumizi yake ya teknolojia ya
mawasiliano na habari.
Mashindano
hayo ya Insha ya Mwaka 2014 yalianzishwa rasmi Oktoba, 2013 ambako
washindani walitakiwa kuandika Insha kuhusu mada: “Climate Change is
having adverse effect on the socio-economic development in the Region.
What should the Education Sector do to mitigate the impact on the youth”
– Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi
ya Kanda ya SADC. Nini Sekta ya Elimu ifanye kupunguza athari hizo kwa
vijana?
Insha
39 zilipokelewa kutoka nchi 13 kati ya nchi 15 wanachama wa SADC ikiwa
ni Insha tatu kwa kila nchi. Insha zilipokelewa kutoka Tanzania, Angola,
Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Lesotho, Malawi,
Mauritius, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na
Zimbabwe.
Majaji
wa kupitia na kuamua washindi wa Insha hizo walitoka Tanzania, Zambia
na Zimbabwe na walikutana mjini Gaborone, Botswana, Julai, mwaka huu
kupitia Insha zote na kutoa uamuzi wa nani washindi.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa SADC umepokea kwa furaha ushindi wa msichana Neema ukieleza kuwa ushindi huo umeiletea Tanzania heshima kubwa katika eneo la SADC na nje ya eneo hilo.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa SADC umepokea kwa furaha ushindi wa msichana Neema ukieleza kuwa ushindi huo umeiletea Tanzania heshima kubwa katika eneo la SADC na nje ya eneo hilo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
17 Agosti,2014
0 Comments