MCHEZAJI Filamu nyota wa kike nchini nchini, Wastara Juma
amesema anakutana na changamoto nyingi katika kuandaa filamu zake tangu
alipofiwa na mume wake mpendwa, Sajuki Juma aliyekuwa msaada mkubwa kwake.
Sajuki alifariki
Dunia Januari 2, 2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa
kwaajili ya matibabu akisumbuliwa na uvimbe pembeni ya ini.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam juzi, Wastara alisema, kutokana na kukutana na changamoto
nyingi katika kazi zake, ameamua kutafuata meneja ambaye wanatasidiana.
“Tangu nimefiwa
filamu ambazo nimefanya mwenyewe ni kama mbili tu, changamoto zilizopo kwangu
ninafanya kazi peke yangu kazi zinakuwa nyingi na sina msaada,”.
“Nimeamua
kumtafuta meneja ambaye atanisaidia baadhi ya kazi muhimu kwasababu watu
wanahitaji kazi nzuri kwa hali hiyo imenilazimu nitafute mtu wa kusaidiana
nae,” alisema.
Aidha, Wastara
alikanusha uvumi wa kwamba amechumbiwa na kwamba bado anamkumbuka mumewe,
Sajuki hivyo kwasasa hana mpango tena wa kuolewa labda hapo baadae.
0 Comments