LIONEL MESSI AIBUKA KIDUME TUZO YA MCHEZAJI BORA KOMBE LA DUNIA 2014

Scant consolation: Lionel Messi was awarded the Golden Ball trophy for player of the tournament


Imechapishwa Julai 14, 2014, saa 8:32 usiku

LICHA ya kupoteza mechi ya fainali na kukosa kombe la dunia mwaka 2014, mshambuliaji wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Tuzo hii imekuja kaka ya kustaajabisha kwa watu wengi, lakini kwa kiasi kikubwa alistahili kupewa.
 Messi alionesha kiwango kikubwa katika hatua ya makundi akifunga mabao 4 katika michezo mitatu dhidi ya Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota yake ilififia baada ya kushindwa kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja muhimu, lakini muda mwingi alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila mafanikio.
Coat of paint: Lionel Messi shoots narrowly wide to miss opening the scoring for Argentina in the Maracana
 Lionel Messi alipiga shuti, lakini alikosa bao katika mchezo wa fainali Maracana.
Baada ya kipyenga cha mwisho, Messi alipokea tuzo yake ya mchezaji bora akiwashinda  nyota wa Colombia James Rodriguez, winga wa Uholanzi, Arjen Robben na wachezaji watatu wa Ujerumani, Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller. 
Dream is over: Lionel Messi looks to the ground after Germany win the World Cup at the Maracana
Ndoto zimezima: Lionel Messi akiangalia chini baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani.

Post a Comment

0 Comments